Featured Kitaifa

VIJANA NCHINI WATAKIWA KUTUNZA  AMANI,UZALENDO NA MSHIKAMANO KWA TAIFA

Written by mzalendoeditor
NAIBU Makamu Mkuu wa Chuo cha Dodoma (UDOM) Prof.Razack Lokina,akizungumza wakati akifungua  mdahalo wa Vijana Kuhusu maadili nchini kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi,Ajira,Vijana na Watu wenye ulemavu Mhe.Ridhiwani Kikwete,uliofanyika jijini Dodoma.

SEHEMU ya Washiriki wakimsikiliza Naibu  Makamu Mkuu wa Chuo cha Dodoma (UDOM) Prof.Razack Lokina (hayupo pichani)wakati akifungua  mdahalo wa Vijana Kuhusu maadili nchini kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi,Ajira,Vijana na Watu wenye ulemavu Mhe.Ridhiwani Kikwete,uliofanyika jijini Dodoma.

Na.Alex Sonna-DODOMA
SERIKALI imewasisitiza vijana kuendelea kutunza  amani, uzalendo na mshikamano kwa Taifa hususan katika kipindi cha uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani.
Hayo yalibainishwa jijini Dodoma  na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi,Ajira,Vijana na Watu wenye ulemavu Mhe.Ridhiwani Kikwete katika hotuba iliyosomwa kwa niaba yake  na Naibu Makamu Mkuu wa Chuo cha Dodoma (UDOM) Prof.Razack Lokina ,wakati akifungua Mdahalo wa Vijana Kuhusu maadili nchini .
alisema  hatma ya Tanzania iko mikononi mwa vijana wazalendo na wenye maadili.
“Tukawe mfano katika kuhubiri na kuishi umoja na mshikamano wa kitaifa hususani tunapoelekea kwenye uchaguzi wa Rais, Wabunge na madiwani mwaka huu wa 2025 tukumbuke kwamba kubomoa umeoja na mshikamano ulijengwa kwa moyo wa dhati na waasisi wetu hii ni kukosa uaminifu na uzalendo kwa taifa letu,”
Aliongeza kuwa :”Kama taifa na kupitia wizara ninayoiongoza iliyopewa dhamana ya masuala ya kazi, vijana, ajira na watu wenye ulemavu tumejipanga katika kuhakikisha kuwa tunatoa kila aina ya uwezeshaji kwenye kuwezesha vijana kujitambua na kushiriki kwenye ujenzi wa taifa letu,.
kwa mujibu wa Ridhiwani alifafanua kuwa  baba wa taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere alisisitiza vijana wana nafasi kubwa katika kujenga mustakali wa taifa la Tanzania na bara la Afrika kwa ujumla lakini nafasi hiyo haitaweza kuwa na tija iwapo vijana hawatazingatia elimu, maadali, umoja na uwajibikaji wa kijamii.
Aidha aliwasisitiza  kubeba maudhui  hayo na  kudumisha na kuhamasisha maadili na uzalendo kwa vijana kwani ni  ni sifa nzuri ambazo zinaweza kuandaa viongozi wa kulitumikia taifa katika misingi ya uwajibikaji.
“Jamii yoyote iliyostaarabika lazima izingatie kuyashika maadili ili kuwezesha uadilifu na uaminifu. Hili ni la muhimu sana kwa kuwa viongozi wenye maadili hufanya maamuzi kwa uaminifu haki na heshima na mwishowe kuwezesha jamii kuishi kwa maelewano na mshikamano.
Aliongeza kuwa :”Uzalendo ni nguzo kubwa katika kuleta umoja unaohitajika katika kufanikisha malengo ya pamoja na ya kitaifa, vijana tunapaswa kuwa wazalendo ili kuweka ubinafsi pembeni kwanza na kushiriki kikamilifu katika kutimiza ndoto kubwa za kitaifa kupitia maona ya viongozi wetu.
Kwa upande wake Kiongozi wa Serikali ya Wanafunzi Chuo Kikuu cha Dodoma Gavana Abisalom Phares Ossere,amesema kuwa lengo la kuandaa komangamono hilo ni kutoa elimu kwa vijana dhidi ya maadili na uzalendo kwa lengo la kupunguza mmonyoko wa maadili kwa vijana.
“Tumefanya hivi kuwakusanya vijana pamoja katika kujadili masuala yanahusu maadili na uzalendo na hii ni kutokana na jamii yetu na jamii zilivyobadilika na masuala ya Sayansi na Teknolojia,Mmomonyoko wa maadili umekuwa kwa asilimia kubwa hivyo kupitia makongamano kama hayo itasaidia kupunguza “amesema 

About the author

mzalendoeditor