Featured Kitaifa

WIZARA YA AFYA YAPOKEA MAGODODRO NA MASHUKA KUTOKA DIASPORA

Written by mzalendoeditor

Waziri wa Afya Zanzibar Mhe, Nassor Ahmesd Mazrui akipokea msaada wa Magodoro na Mashuka kwaajili ya hospitali za Zanzibar, wenye thamani ya zaid ya shilingi milioni 13 kutoka kwa Wazanzibar waishio Nchi za Umoja wa falme za kiarabu (Diaspora) huko Ofisini kwake Mnazimmoja Mjini Unguja.

 

PICHA NA FAUZIA MUSSA –MAELEZO ZANZIBAR.

…………………………………………

NA SABIHA KHAMIS  -MAELEZO

Wizara ya Afya imepokea msaada wa mashuka na magodoro wenye thamani ya ya zaidi milioni 13 kutoka Umoja wa Wazanzibar wanaoishi katika Falme za kiarabu (Diaspora) wenye lengo la kuleta maendeleo katika sekta ya Afya.

Akizungumza mara baada ya kupokea msaada huo Waziri wa Afya Mhe Nassor Ahmed Mazrui huko ofisini kwake Mnazi Mmoja, amesema msaada huo utasaidia kuboresha na kuimarisha utoaji wa huduma za afya nchini

Ameushukuru Umoja huo kwa kuonesha uzalendo wa kuipenda nchi yao na kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Wizara ya Afya katika kutoa huduma bora kwa wananchi.

Aidha Waziri Mazrui, ameahidi kuusimamia vyema msaada huo na kuhakikisha kwamba unatumika ipasavyo, pomoja na kuutunza ili uweze kutumika na  kudumu kwa muda mrefu.

“Niwahakikishie kuwa nitausimamia mzigo huu ili uwafikie walengwa wanaostahiki kutumia magodoro na mashuka hayo pamoja na kuyatunza ili kuishi kwa muda mrefu”, alieleza Waziri.

Nae Mwakilishi wa umoja huo Mohamed Khamis (Edi Kalipso) amesema kuwa wataendelea kuisaidia sekta ya afya pamoja kuwaomba Wazanzibar wengine kujitokeza kusaidia ili kuhakikisha kwamba utoaji wa huduma  unaimarika nchini.

About the author

mzalendoeditor