Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) Mhandisi Peter Mwasalyanda,akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio na mwelekeo wa taasisi hiyo katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Sita leo Machi 27, 2025, katika Ofisi za Idara ya Habari – MAELEZO, jijini Dodoma
Sehemu ya Waandishi wa habari wakimsikiliza Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) Mhandisi Peter Mwasalyanda,(hayupo pichani) wakati akiwasilisha mafanikio na mwelekeo wa taasisi hiyo katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Sita leo Machi 27, 2025, katika Ofisi za Idara ya Habari – MAELEZO, jijini Dodoma.
“Pamoja na mradi huo pia tumeboresha minara 304 kuiongezea nguvu kutoka kwenye 2G hadi 3G kwa gharama ya zaidi ya bilioni 5,”
Na kuongeza kuwa “Dhamira ya serikali ni kuona wanachi hawapati changamoto ya Mawasiliano kwani bila Mawasiliano mazuri hata suala la ukuaji wa uchumi utakuwa mdogo kwani biashara nyingi kwa sasa zinategemea mtandao madhubuti hivyo jitihada hizi za kuboresha Mawasiliano nchini zinalenga kuchochea maendeleo, “amesema Mhandisi Mwasalyanda
Mhandisi Mwasalyanda amesema Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Uongozi wa Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri inatambua umuhimu wa shirika la Posta nchini na hivyo katika kipindi cha miaka minne Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote imekuwa ikiliwezesha shirika la Posta kwa kulipatia vifaa vya TEHAMA ili shirika liweze kutoa huduma kidigitali.
Ambapo tarehe 12 Julai 2024, UCSAF ilinunua PDA 250 na kuwakabidhi Shirika la Posta. Gharama za utekelezaji wa mradi huu ni kiasi cha TZS 161,926,471/=.
Mwezi Aprili 2025, UCSAF itakabidhi vifaa vingine 250 kwa shirika la Posta vyenye thamani ya TZS 161,926,471/=