Featured Kitaifa

UWT YAFANYA DUA YA SHUKRANI NA KUMUOMBEA RAIS DKT. SAMIA KWA UONGOZI ULIOSTAWISHA NCHI

Written by mzalendo

Na Mwandishi Wetu. 

Jumuiya ya Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi Tanzania (UWT) imefanya Dua Maalum ya Shukrani na Kumuombea Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa Uongozi wake katika kipindi cha Miaka Minne ulioleta maendeleo kwa nchi toka alipoapishwa kuwa Rais Machi 19, 2021.

Viongozi waandamizi wa UWT wakiongozwa na *Mwenyekiti wa Taifa Ndg. Mary Pius Chatanda (MCC)* pamoja Viongozi mbalimbali wa Chama na Jumuiya ya UWT,Viongozi wa Serikali wa Mikoa ya Dar es Salaam na Pwani waliungana kwa pamoja kumuombea Rais Samia kuendelea kuiongoza nchi kwa amani pamoja kutekeleza majukumu yake yenye kuleta maendeleo kwa ustawi wa nchi.

Dua hiyo iliyoambatana na hafla ya Iftar kwa makundi mbalimbali wakiwemo wanafunzi wa Madrasat na waumini wa Dini ya kiislam,imefanyika katika Viwanja vya Karimjee Jijini Dar es Salaam leo jioni Machi 20, 2025.

Akizungumza baada ya Dua hiyo, Mwenyekiti Chatanda ametoa wito kwa Watanzania hususani Wanawake kuendelea kumuunga Mkono Rais Samia kutokana na dhamira yake Njema ya kuwaletea Watanzania maendeleo.

“Sisi UWT tumeamua kumfanyia Dua mpendwa wetu Rais Samia kutokana na mambo makubwa aliyofanya na sisi Wanawake ni mashuhuda wakubwa”

Tumeona Rais ameimarisha Sekta ya Afya kwa kujenga na kuboresha vituo vya Afya,Zahanati na Hospitali za Wilaya na za Rufaa pamoja na uwepo wa Vifaa Tiba,na yote hayo ameyafanya katika Sekta ya Maji na Elimu”

“Hivyo UWT tuna kila sababu ya kumshukuru na kumuombea na niendelee kutoa wito tujitokeze kujiandikisha kwenye Daftari la Wapiga Kura linaloendelea katika Mkoa wa Dar es Salaam ili itakapofika Mwezi Oktoba tumchague na kumpa ushindi wa kishindo Mpendwa wetu Rais Samia”

About the author

mzalendo