Featured Kitaifa

MIAKA 4 YA RAIS SAMIA ALIVYOTEKELEZA HAKI ZA BINADAMU

Written by mzalendoeditor

Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro ameeleza jinsi ambavyo katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ametekekeleza kwa vitendo haki za binadamu

Waziri Ndumbaro amesema hayo Leo Machi 19, 2025 Jijini Dar Es Salaam wakati wa ufunguzi wa kikao kazi cha kupitia mkataba wa Afrika wa haki za binadamu na watu pamoja na itifaki ya maputo.

Amesema kuwa kupitia falsafa ya 4R imewezesha serikali ya awamu ya sita kutekeleza kwa vitendo haki za binadamu yaani, Maridhiano, Ustahimilivu, Mageuzi na Kujenga upya.

Kwa Upande wake Mkurugenzi msaidizi wa Haki za Binadamu kutoka Wizara ta Katiba na Sheria Bi. Beatrice Mpembo amesema kuwa kikao hicho kitapitia na kujadili hatua zilizochukuliwa na serikali katika utekelezaji wa mkataba wa Afrika wa haki za binadamu na watu pamoja na itifaki ya haki za wanawake Afrika.

Jumla ya asasi 13 za kiraia zinashiriki katika kikao hicho ambacho kitatoa mwelekeo wa juhudi za kulinda haki za binadamu nchini na kukuza ustawi wa wanawake.

About the author

mzalendoeditor