Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Bw. Mavere Tukai akizungumza na waandishi wa habari leo Machi 17,2025 katika Ofisi za Idara ya Habari – MAELEZO, jijini Dodoma kuhusu mafanikio na mwelekeo wa Bohari ya Dawa katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Sita.
Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Bw. Mavere Tukai akizungumza na waandishi wa habari leo Machi 17,2025 katika Ofisi za Idara ya Habari – MAELEZO, jijini Dodoma kuhusu mafanikio na mwelekeo wa Bohari ya Dawa katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Sita.
Na.Alex Sonna-DODOMA
SERIKALI imeiwezesha Bohari ya Dawa (MSD) kukamilisha ujenzi wa Kiwanda pekee cha kuzalisha mipira ya mikono “Gloves” kilichopo Halmashauri ya Mji Makambako, Mkoani Njombe na kuanza uzalishaji.
Hayo yamesemwa leo Machi 19,2025 na Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Bw. Mavere Tukai,wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio na mwelekeo wa Bohari ya Dawa katika kipindi cha miaka minne chini ya Uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan.
Amesema kuwa Kiwanda hicho kimegharimu a kiasi cha shilingi bilioni 16 kutoka Serikali, Kiwanda hicho kina uwezo wa kuzalisha wastani wa Gloves milioni 24.4 na kusaidia kukidhi zaidi ya asilimia 60 ya mahitaji ya bidhaa hii nchini na kupunguza uagizaji wa bidhaa hiyo kutoka nje ya nchi.
“Viwanda hivyo kwa sasa vipo chini ya Kampuni Tanzu ya MSD, MSD Medipharm Manufacturing Company Limited ambayo inasimamia Kiwanda cha Mipira ya Mikono Idofi – Njombe, eneo la viwanda la Zegereni – Pwani na Kiwanda cha Barakoa – Dar es Salaam pamoja na viwanda vya bidhaa za Afya zitokanazo na malighafi ya pamba na hivyo kupunguza uagiazaji wa bidhaa zitokanazo na pamba ambazo hugharimu nchini zaidi ya shilingi bilioni 25.”amesema Bw. Mavere
Aidha amesema kuwa hadi kufikia mwezi Februari 2025, Kiwanda kimeweza kuzalisha jumla ya gloves zaidi ya milioni 5.6 zenye thamani ya shilingi bilioni 1.9 ambapo mpaka sasa gloves zenye thamani ya shilingi 709,597,840 zimeshaingizwa sokoni na zitaendelea kuingizwa sokoni.
“Kutokana na uwepo wa kiwanda hicho , Bohari ya Dawa imeanza mkakati wa kuhimiza uzalishaji wa utomvu nchini wa kiwango kinachostahili ili malighafi zote za kiwanda hicho ziweze kupatikana nchini hivyo kuongeza wigo wa ajira na kupunguza matumizi ya fedha zinazotumika kuagiza malighafi hizo.
“amesema
Amesema kuwa Mnamo mwezi Oktoba 2024, Kampuni Tanzu ya Bohari ya Dawa inayoitwa MSD
Medipharm Manufacturing Company Limited ilifanikiwa kusaini makubaliano ya uzalishaji wa bidhaa za afya kwa njia ya Joint Venture na Kampuni ya Rotabiogen East Africa inayomilikiwa na Kampuni ya Rotabiogen Egypt ya nchini Misri.
Amesema kuwa lengo la kufanya uwekezaji na kuanza uzalishaji wa dawa za binadamu katika eneo la MSD lilipo Zegereni (Industrial Park for health commodities) na hivyo kwa pamoja kuanzisha
Kampuni inayoitwa ROTAMEDI CO.LTD kwa utekelezaji wa mradi huu.
“Gharama za mradi huu zinatarajia kufika shilingi bilioni 183.3, sawa na Dola za Kimarekani milioni
72. Utekelezaji wa mradi huu umeanza mwezi Januari 2025 ambapo wataalamu kutoka Misri wamefika Tanzania na kukagua eneo la mradi na kuchukua taarifa kwa ajili ya kuanza usanifu wa mradi.”amesema
Hata hivyo amesema kuwa Viwanda hivyo vitakapokamilika vitapunguza uagizaji wa bidhaa za afya kutoka nje ya nchi zenye thamani ya shilingi bilioni 35 kwa mwaka, kutoa mafunzo na ajira kwa Watanzania juu ya uzalishaji wa bidhaa za afya.
Kampuni Tanzu ya MSD inaendelea kukamilisha uchambuzi wa athari za kimazingira (Enviromental and Social impact assessment) la eneo la mradi kama inavyoelekezwa na Baraza la Usimamizi wa mazingira (NEMC).