Featured Kitaifa

RAIS SAMIA KUZINDUA SERA MPYA YA ARDHI TOLEO LA 2023.

Written by mzalendoeditor

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Deogratius Ndejembi,akizungumza na  waandishi wa habari (hawapo pichani)  leo Machi 17,2025 jijini Dodoma kuelekea uzinduzi wa Sera ya Ardhi ya Mwaka 1995, toleo la 2023, unatafanyika Machi 17,mwaka huu katika ukumbi wa Jakaya Kikwete.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Deogratius Ndejembi,akizungumza na  waandishi wa habari (hawapo pichani)  leo Machi 17,2025 jijini Dodoma kuelekea uzinduzi wa Sera ya Ardhi ya Mwaka 1995, toleo la 2023, unatafanyika Machi 17,mwaka huu katika ukumbi wa Jakaya Kikwete.

Na.Alex Sonna-DODOMA
RAIS Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuzindua Sera ya Ardhi ya Mwaka 1995, toleo la 2023 ambayo inayolenga kukidhi mahitaji ya sasa na kugusa masuala mbalimbali ikiwamo migogoro ya ardhi.
Akizungumza  na waandishi wa habari leo Machi 17,2025 jijini Dodoma, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Deogratius Ndejembi, amesema kuwa uzinduzi huo unatafanyika Machi 17,mwaka huu katika ukumbi wa Jakaya Kikwete.
Mhe.Ndejembi, amesema maandalizi ya uzinduzi huo yamekamilika kwa asilimia 90, na kazi zilizobaki zitakamilika ndani ya siku muda mfupi.
“Kutokana na umuhimu wa suara la ardhi, miongoni mwa wageni watakaohudhuria ni pamoja na Mabalozi wa nchi mbalimbali, Wakuu wa Mikoa pamoja na  Mawaziri.”amesema Mhe.Ndejembi
 Sera hii inalenga kuimarisha usimamizi wa ardhi kwa kuongeza ufanisi wa utawala, kutatua migogoro ya ardhi, na kuweka mifumo inayosomana ili kurahisisha upatikanaji wa taarifa na ufuatiliaji wa shughuli za ardhi.
Pia, itaongeza uwazi na ushirikishwaji wa wananchi katika masuala ya ardhi, kuwezesha uwekezaji endelevu, na kulinda haki za wamiliki wa ardhi vijijini na mijini.
Kaulimbiu ya uzinduzi huo ni “Sera ya Ardhi Msingi wa Ustawi na Malengo Endelevu ya Taifa”

About the author

mzalendoeditor