Featured Kitaifa

MATUMIZI SAHIHI MFUMO WA KIDIGITALI KUONGEZA UFANISI KATIKA VYAMA VYA USHIRIKA TANZANIA BARA NA ZANZIBAR 

Written by mzalendoeditor
MRAJIS  na Mtendaji Mkuu Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC), Dkt. Benson Ndiege,akizungumza  wakati akifungua kikao kazi cha kujenga mahusiano ya karibu na kuweka mikakati juu ya matumizi ya Mfumo wa Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (MUVU) na  Idara  Maendeleo ya Ushirika Zanzibar.
Na.Alex Sonna-DODOMA
TUME  ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC) imekutana na Idara  Maendeleo ya Ushirika Zanzibar kuweka mikakati  ya mahusiano na mafunzo kuhusu matumizi sahihi ya mfumo wa kidigitali ili kuongeza ufanisi wa utendaji kazi katika Vyama vya Ushirika Tanzania Bara na  Zanzibar.
Hayo yameelezwa leo Machi 10,2025 jijini Dodoma na Mrajis na Mtendaji Mkuu Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC), Dkt. Benson Ndiege,wakati wa ufunguzi wa kikao kazi cha kujenga mahusiano ya karibu na kuweka mikakati juu ya matumizi ya Mfumo wa Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (MUVU).
Dkt. Ndiege amesema kuwa mikakati madhubuti juu ya  matumizi sahihi ya  mfumo wa kidigitali itasaidia kuongeza ufanisi wa utendaji kazi wa Vyama vya Ushirika na kuleta matokeo chanya kwa wachama wa Vyama vya Ushirika Tanzania na Zanzibar
“Mpaka sasa zaidi ya vyama 6,000 vimesajiliwa kwenye mfumo wa kidigitali na viko hai  na Vinahudumia wanachama wake walio sajiliwa kwenye mfumo huo,” amesema  Dkt. Ndiege.
Vile vile Dkt Ndiege amesema kuwa vyama vilivyosajiliwa katika Mfumo wa kidigitali ndiyo Vyama vinavyoruhusiwa kufanya kazi ili kuleta ufanisi kwenye Ushirika kwa wanachama wake kwasababu hata data za Wanachama zinapatikana kwa uhakika kwenye Mfumo.
Kwa upande wake kiongozi wa Msafara kutoka Zanzibar, Mkurugenzi Uendeshaji na Utumishi kutoka Ofisi ya Rais, Kazi, Uchumi na Uwekezaji Bw.Mohammed Jaffar Jumanne , amesema kuwa wameambatana na idara ya ushirika katika ziara ya mashirikiano kwa lengo la kubadilishana uzoefu, elimu na kuona ubora wa utendaji kazi ili kuongeza ujuzi katika kuendesha shughuli za Ushirika .
Kwa upande wake Kaimu Mrajis Idara ya Maendeleo ya Ushirika Zanzibar, Zainab Abdullkadiri, amesema  wamekuwa na ushirikiano wa kutosha na TCDC kwa muda mrefu ila ushirikiano huo haukuwa rasmi.
“Hivyo kupitia Ziara ya kikazi hii tunatarajia kurasimisha ushirikiano wetu na TCDC kwa kusaini makubaliano ya kufanya kazi baina ya Tanzania bara na Visiwani ambapo makubaliano hayo yatasainiwa rasmi siku ya Jumatano na makatibu Wakuu wote wawili,” amesema Zainab.

MRAJIS  na Mtendaji Mkuu Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC), Dkt. Benson Ndiege,akizungumza  wakati akifungua kikao kazi cha kujenga mahusiano ya karibu na kuweka mikakati juu ya matumizi ya Mfumo wa Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (MUVU) na  Idara  Maendeleo ya Ushirika Zanzibar,kilichofanyika leo Machi 10,2025 jijini Dodoma.
KIONGOZI  wa Msafara kutoka Zanzibar, Mkurugenzi Uendeshaji na Utumishi kutoka Ofisi ya Rais, Kazi, Uchumi na Uwekezaji Bw.Mohammed Jaffar Jumanne,akizungumza wakati wa  kikao kazi cha kujenga mahusiano ya karibu na kuweka mikakati juu ya matumizi ya Mfumo wa Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (MUVU) kati ya Tanzania bara na Zanzibar,kilichofanyika leo Machi 10,2025 jijini Dodoma.

KAIMU  Mrajis Idara ya Maendeleo ya Ushirika Zanzibar, Zainab Abdullkadiri,,akizungumza wakati wa  kikao kazi cha kujenga mahusiano ya karibu na kuweka mikakati juu ya matumizi ya Mfumo wa Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (MUVU) kati ya Tanzania bara na Zanzibar ,kilichofanyika leo Machi 10,2025 jijini Dodoma.

About the author

mzalendoeditor