Featured Kitaifa

WORLD VISION TANZANIA YAKABIDHI VIFAA VYA KILIMO, UFUGAJI NYUKI NA LISHE VYA MILIONI 97.6 SHINYANGA

Written by mzalendoeditor
Kaimu Meneja wa World Vision Tanzania Kanda ya Ziwa, Shukrani Dickson ( wa pili kushoto) akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha vifaa mbalimbali vya Kilimo, ufugaji nyuki na lishe kwa ajili ya kuboresha uchumi wa kaya na lishe wilayani Kishapu
 

Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog

 
Shirika la World Vision Tanzania limekabidhi vifaa vyenye thamani ya shilingi milioni 97.6 kwa serikali ya mkoa wa Shinyanga ikiwa ni sehemu utekelezaji wa mradi wa NOURISH unaotekelezwa wilayani Kishapu.
 
Vifaa hivi vinajumuisha mizinga ya nyuki, pampu za umwagiliaji, mbegu za mazao, mashine za kukamulia asali, na vifaa vya kuhifadhi mazao, vyote vikiwa na lengo la kuboresha uchumi wa kaya, lishe ya familia, na kuongeza uzalishaji wa mazao katika kata za Lagana, Ngofila na Mwamashele wilayani Kishapu.
 
Hafla ya makabidhiano imefanyika Februari 4, 2025 mjini Shinyanga, ambapo Mgeni Rasmi, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Anamringi Macha, ameongoza tukio hili muhimu.
 
Vifaa vilivyokabidhiwa vinategemewa kusaidia wakulima na familia katika wilaya ya Kishapu, ikiwa ni juhudi za pamoja kati ya shirika la World Vision na serikali ya mkoa katika kuboresha hali ya maisha, hasa kwa watoto na familia zinazokabiliwa na changamoto za lishe na upatikanaji wa chakula.

 

Muonekano wa sehemu vifaa vilivyotolewa na Shirika la World Vision Tanzania

 

Kaimu Meneja wa World Vision Tanzania Kanda ya Ziwa, Shukrani Dickson, ameeleza kuwa, Vifaa vilivyokabidhiwa ni sehemu ya juhudi za shirika kuboresha upatikanaji wa chakula na lishe bora kwa familia, hasa watoto wanaoishi katika mazingira magumu.
 
Amefafanua kuwa vifaa hivyo vimetolewa kupitia mradi wa NOURISH unaofadhiliwa na nchi ya Ireland. Mradi huu unafanya kazi ya kuboresha lishe, uzalishaji mali na kuongeza kipato kwenye kaya pamoja na kuwezesha jamii kupata elimu ya kukabiliana na maafa katika Wilaya ya Kishapu, kwa kushirikiana na Shirika la KIVULINI ambao wanafanya kazi katika sekta ya usawa wa kijinsia.

 

Kaimu Meneja wa World Vision Tanzania Kanda ya Ziwa, Shukrani Dickson (katikati) akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha vifaa mbalimbali vya Kilimo, ufugaji nyuki na lishe kwa ajili ya kuboresha uchumi wa kaya na lishe wilayani Kishapu

 

Ameeleza kuwa , vifaa vilivyokabidhiwa vinajumuisha Mizinga ya nyuki, vifaa vya kurinia asali na mashine ya kukamulia asali,mifuko ya kinga njaa, pampu za umwagiliaji, mbegu za mboga mboga na mazao, mbolea za kupanda na kukuzia, miti ya matunda, mashine ya umeme ya kukaushia mazao ya mbogamboga na vifaa vya kujengea friji ya asili ya kutunza mazao ya mbogamboga vyenye thamani ya shilingi 97,649,200/= vyote vikiwa na lengo la kuboresha kilimo na kuongeza tija katika uzalishaji wa chakula.
 
“Mradi huu ni muhimu sana kwa sababu unalenga kuhakikisha jamii yetu inapata chakula cha kutosha na bora, na pia tunawawezesha wanawake na vijana kupitia shughuli za kilimo na biashara ya mazao,” amesema Shukrani.
 
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Macha, amelishukuru shirika la World Vision kwa mchango wake, akisema kuwa vifaa hivi vitasaidia sana katika kuboresha uchumi wa wananchi na kuongeza tija katika sekta ya kilimo.
“World Vision Tanzania ni taasisi inayotoa michango yenye mashiko na manufaa kwa jamii. Tunashukuru kwa namna inavyoshirikiana na serikali kuboresha maisha ya wananchi. Shukrani za pekee ziende kwa Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa uongozi wake mzuri ambao umeweka mazingira rafiki kwa wadau mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi kufanya shughuli zinazolenga kuwaletea maendeleo wananchi,” amesema Mhe. Macha.
 
Amewataka wakulima na wananchi kutumia vifaa hivi kwa manufaa yao, na ameahidi kutembelea kata za Lagana, Mwamashele, na Ngofila ili kujionea maendeleo yatakayopatikana kutokana na vifaa hivi.
 
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Mhe. Peter Masindi, amesema kuwa vifaa hivi vitachochea maendeleo na kuleta mapinduzi katika kilimo cha kibiashara katika wilaya hiyo.
 
Ametoa wito kwa wadau wengine kuendelea kushirikiana na serikali ili kuhakikisha wananchi wanapata fursa za kiuchumi.

 

Wanufaika wa vifaa hivi wameeleza shukrani zao kwa World Vision na serikali kwa ushirikiano wao, wakiahidi kutumia vifaa hivyo kujiletea maendeleo na kuboresha maisha yao.

 

 
Shirika la World Vision Tanzania linajivunia miradi yake inayotekelezwa katika mikoa mbalimbali ya Tanzania, likifanya kazi kwa karibu na jamii na serikali katika kuboresha huduma za afya, elimu, lishe, uzalishaji mali, na haki za kijinsia.
 
Katika mkoa wa Shinyanga Shirika la World Vision lina miradi katika wilaya 3 za Shinyanga, Kishapu na Kahama likishirikiana na serikali na jamii kutoa huduma za jamii. Miradi hiyo ni Mpango wa Eneo Kilago uliopo Kahama, Mpango wa eneo Mwakipoya, Mpango wa eneo Lagana, Mradi wa NOURISH upo Kishapu na GROW ENRICH inafanya kazi katika wilaya mbili za Kishapu na Shinyanga.
 
Shirika la World Vision Tanzania ni Shirika la Kikristo la maendeleo, misaada na utetezi, lisilo la kiserikali ambalo limejikita kufanya kazi na watoto, familia, na jamii ili kupambana na umasikini na ukosefu wa haki.

 

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Anamringi Macha akizungumza wakati Shirika la World Vision Tanzania likikabidhi vifaa mbalimbali vya Kilimo, ufugaji nyuki na lishe kwa ajili ya kuboresha uchumi wa kaya na lishe wilayani Kishapu
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Anamringi Macha akizungumza wakati Shirika la World Vision Tanzania likikabidhi vifaa mbalimbali vya Kilimo, ufugaji nyuki na lishe kwa ajili ya kuboresha uchumi wa kaya na lishe wilayani Kishapu
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Anamringi Macha akizungumza wakati Shirika la World Vision Tanzania likikabidhi vifaa mbalimbali vya Kilimo, ufugaji nyuki na lishe kwa ajili ya kuboresha uchumi wa kaya na lishe wilayani Kishapu

 

Kaimu Meneja wa World Vision Tanzania Kanda ya Ziwa, Shukrani Dickson akizungumza wakati akikabidhi vifaa mbalimbali vya Kilimo, ufugaji nyuki na lishe kwa ajili ya kuboresha uchumi wa kaya na lishe wilayani Kishapu
Kaimu Meneja wa World Vision Tanzania Kanda ya Ziwa, Shukrani Dickson akizungumza wakati akikabidhi vifaa mbalimbali vya Kilimo, ufugaji nyuki na lishe kwa ajili ya kuboresha uchumi wa kaya na lishe wilayani Kishapu
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mhe. Peter Masindi akizungumza wakati Shirika la World Vision Tanzania likikabidhi vifaa mbalimbali vya Kilimo, ufugaji nyuki na lishe kwa ajili ya kuboresha uchumi wa kaya na lishe wilayani Kishapu
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Wakili Julius Mtatiro akizungumza wakati Shirika la World Vision Tanzania likikabidhi vifaa mbalimbali vya Kilimo, ufugaji nyuki na lishe kwa ajili ya kuboresha uchumi wa kaya na lishe wilayani Kishapu
Kaimu Meneja wa World Vision Tanzania Kanda ya Ziwa, Shukrani Dickson ( kulia) akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha vifaa vya kurinia asali
Muonekano wa sehemu vifaa mbalimbali vya Kilimo, ufugaji nyuki na lishe vilivyotolewa na Shirika la World Vision Tanzania kwa ajili ya kuboresha uchumi wa kaya na lishe wilayani Kishapu
Muonekano wa sehemu vifaa mbalimbali vya Kilimo, ufugaji nyuki na lishe vilivyotolewa na Shirika la World Vision Tanzania kwa ajili ya kuboresha uchumi wa kaya na lishe wilayani Kishapu
Mwezeshaji wa Mradi wa NOURISH, Proches Lyimo (kulia) akimuonesha Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha sehemu vifaa mbalimbali vya Kilimo, ufugaji nyuki na lishe vilivyotolewa na Shirika la World Vision Tanzania kwa ajili ya kuboresha uchumi wa kaya na lishe wilayani Kishapu
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mhe. Peter Masindi akizungumza wakati Shirika la World Vision Tanzania likikabidhi vifaa mbalimbali vya Kilimo, ufugaji nyuki na lishe kwa ajili ya kuboresha uchumi wa kaya na lishe wilayani Kishapu
 
Wanufaika wa vifaa mbalimbali vya Kilimo, ufugaji nyuki na lishe vilivyotolewa na Shirika la World Vision Tanzania wakipiga picha ya pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha

About the author

mzalendoeditor