Featured Kitaifa

WANANCHI WA WILAYA YA SAME WASHAURIWA KUTUMIA WATOA HUDUMA ZA FEDHA WALIO SAJILIWA

Written by mzalendoeditor
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Same, Bw. Jimson Mhagama akizungumza na Timu ya Wataalam wa kutoa Elimu ya Fedha, Kutoka Wizara ya Fedha na Taasisi zake, walipofika Ofisini kwake kabla ya kuanza kutoa elimu ya fedha ikiwa ni mwendelezo wa zoezi la kutoa elimu hiyo kwa wananchi wa makundi mbalimbali katika kata ya Stesheni Wilaya ya Same, Mkoa wa Kilimanjaro.
Mkuu wa Wilaya ya Same, Mhe. Kasilda Mgeni, akiwa katika picha ya pamoja na Timu ya Wataalam wa kutoa Elimu ya Fedha, Kutoka Wizara ya Fedha na Taasisi zake, kwa ajili ya kutoa elimu ya fedha Wilaya ya Same, Mkoa wa Kilimanjaro. Kamishina Msaidizi wa Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha, Bi. Dionesia Mjema (wa pili kushoto), Afisa Usimamizi wa Fedha katika Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha – Wizara ya Fedha, Bw. Stanley Kibakaya (kulia)
 
Kamishina Msaidizi wa Idara ya Uendelezaj wa Sekta ya Fedha, Bi. Dionesia Mjema, akitoa mada kuhusu masuala ya fedha na umuhimu wa kusajili vikundi vya kutoa Huduma Ndogo za Fedha na vile vya kijamii kwa wananchi wa Kata ya Stesheni, kwenye program maalum ya elimu ya fedha iliyotolewa kwa wananchi katika ukumbi wa Shule ya Same Sekondari  Kata ya Stesheni Wilaya ya Same, Mkoa wa Kilimanjaro.
 Afisa Usimamizi wa Fedha katoka Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha – Wizara ya Fedha, Bw. Stanley Kibakaya, akifafanua  kuhusu masuala  ya mikopo salama na umuhimu wa kusajili vikundi vya kutoa Huduma Ndogo ya Fedha kwa wananchi na wanafunzi wa Kata ya Stesheni kwenye program maalum ya elimu ya fedha iliyotolewa katika ukumbi wa Shule ya Same Sekondari Kata ya Stesheni Wilaya ya Same, Mkoa wa Kilimanjaro.

Afisa Usimamizi wa Fedha katoka Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha – Wizara ya Fedha, Bw. Stanley Kibakaya, akigawa vipeperushi vya masuala ya fedha  kuhusu mikopo salama na umuhimu wa kusajili vikundi vya kutoa Huduma Ndogo ya Fedha kwa wananchi na wanafunzi wa Kata ya Stesheni kwenye program maalum ya elimu ya fedha iliyotolewa katika ukumbi wa Shule ya Same Sekondari Kata ya Stesheni Wilaya ya Same, Mkoa wa Kilimanjaro
Picha za matukio mbalimbali ya wananchi wakipatiwa elimu ya fedha katika Wilaya ya Same Mjini  mkoani kilimanjaro, baada ya Timu ya Wataalam kutoka Wizara ya Fedha kwa kushirikiana na Maafisa  kutoka Taasisi  pamoja na wadau mbalimbali walipotembelea na kutoa elimu ya fedha kwa wajasiliamali na  wananchi wa Wilaya hiyo. (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-WF, Same)
…….
Na Chedaiwe Msuya, WF, Same
 
Mkuu wa Wilaya ya Same, Mhe. Kasilda Mgeni, amewaasa watoa huduma za fedha wilayani humo kuhakikisha kuwa wanatii  Sheria zinazosimamia huduma za fedha kwa kusajili huduma zao ili kuweza kutoa huduma za fedha kwa mujibu wa Kanuni, Sheria na Miongozo iliyipo kuwa ni muhimu kwa watoa huduma wote kufuata utaratibu ulioanzishwa na Serikali ili kuzuia watoa huduma wasio waaminifu kwa kutoa mikopo kwa riba kubwa na kuchukua dhamana za wananchi bila kufuata taratibu.
 
Mhe. Mgeni alitoa rai hiyo alipokutana na Timu ya wataalamu kutoka Wizara ya Fedha walipofika wilayani Same kutoa elimu ya fedha kwa Umma.
 
Programu hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa Mpango Mkuu wa Maendeleo ya Sekta ya Fedha wa Wizara ya Fedha wa kutoa elimu ya fedha ambapo moja ya malengo ni kuhakikisha utoaji wa Elimu ya Fedha na kumlinda mlaji ambapo imejiwekea malengo ya kuwafikia asilimia 80 ya Watanzania.
 
“Watoa huduma za fedha wanaoendesha shughuli zao wilayani humu bila kuwa na leseni halali na kuweka riba kubwa kinyume na viwango vinavyokubalika, watakumbana na hatua za kisheria,” Alisisitiza Mhe. Mgeni.
 
Aliongeza kuwa, elimu ya fedha inayotolewa kwa wananchi ni muhimu kwani itawasaidia kuepuka mikopo ya kifedha isiyofaa na kuwajengea uelewa kuhusu umuhimu wa kuweka akiba, ikiwa ni njia mojawapo ya kuhakikisha kuwa wananchi wanapata elimu ya kifedha inayowasaidia kujua jinsi ya kutunza na kutumia fedha zao kwa njia bora.
 
Kamishina Msaidizi wa Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha, Bi. Dionesia Mjema, alizungumzia umuhimu wa elimu ya fedha, akisema kuwa Serikali inatekeleza programu hiyo ili kuwajengea wananchi uwezo wa kufanya maamuzi sahihi kuhusu matumizi ya fedha zao. 
 
“Ni muhimu kuwa na utaratibu wa kuweka akiba na kuhakikisha kuwa mikopo inayochukuliwa inatolewa na taasisi zilizojulikana na kusajiliwa rasmi na Benki Kuu ya Tanzania”, alisema Bi. Mjema.

About the author

mzalendoeditor