Michezo

SIMBA YAICHAPA ORLANDO PIRATES ROBO FAINALI CAF

Written by mzalendoeditor

 

Na Alex Sonna

SIMBA wameendelea kulinda kauli yao kuwa kwa Mkapa Hatoki Mtu baaada ya kuichapa bao 1_0 Orlando Pirates mchezo wa Robo Fainali Kombe la Shirikisho barani Afrika uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam .

Simba walipata bao la ushindi dakika ya 67 likifungwa na beki kisiki Shomari Kapombe kwa Mkwaju wa Penalti baada ya Benerd Morison kuchezewa rafu ndani ya 18 na mwamuzi kuamua kuwa Penalti.

Simba na Orlando watarudiana April 23,2022 mchezo utakaochezwa nchini Afrika Kusini na ndo utaamua nani atinge hatua ya Nusu Fainali.

About the author

mzalendoeditor