Featured Kitaifa

USHINDI WA KISHINDO WA CCM UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA ULITOKANA NA JUHUDI ZA WANA CCM:ISSA GAVU

Written by mzalendo

Na Mwandishi Wetu, Tanga. 

Chama Cha Mapinduzi kimeeleza kuwa ushindi wa kishindo ulioupata kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika Novemba 27, 2024 umetokana na Juhudi za wanachama wa CCM waliokitafutia kura za ushindi tofauti na baadhi ya taasisi mbalimbali zinavyoeleza.

Hayo yameelezwa na Katibu wa NEC,Idara ya Organaizesheni CCM Ndg. Issa Ussi Gavu alipokuwa akifungua Kikao cha Kawaida cha Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) kilichofanyika jijini Tanga leo tarehe 15 Disemba, 2024.

“Kulikuwa na taasisi nyingi nje ya mfumo wa Chama chetu, niwaambie tu kuwa hakuna taasisi,kikundi wa mtu aliyewezesha ushindi wa Chama chetu CCM.Tuliopambana kukitafutia ushindi wa kishindo kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ni sisi wana CCM”

“Nataka Wana CCM tusimame na kujipiga kifua na tuwathibitishie watanzania kuwa Chama chetu hakina shida ya watu kupiga debe,Chama chetu kipokamilifu,kina nyenzo thabiti na Wanachama thabiti.Kama tulivyoshinda kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ndivyo hivyo hivyo tutashinda kwenye Uchaguzi Mkuu 2025”

“Tunaendelea kuwakumbusha kuwa sisi hakukatai kushirikiana na mtu,ila anayehitaji kushirikiana na lazima wafate miongozo na maelekezo yanayotokana na CCM”.

#uwtimara
#jeshiladktsamiadktmwinyi
#Kaziiendelee
#ushindinilazima
#mitanotena
#tukutanekwabalozi
#Miaka63YaUhuru

About the author

mzalendo