Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akipewa maelezo na Mthibiti Ubora wa Kiwanda cha Uzalishaji dawa za Binadamu cha CURE AFYA, Kareem Mruthu, alipotembelea kiwanda hicho kilichopo Kimbiji, Wilaya ya Kigamboni Jijini Dar es Salaam, Desemba 14, 2024. Kushoto ni Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akioneshwa na Mwenyekiti wa Africab Group Ali ezzi baadhi ya dawa zinazotengenezwa katika Kiwanda cha Uzalishaji dawa za Binadamu cha CURE AFYA kilichopo Kimbiji, Wilaya ya Kigamboni Jijini Dar es Salaam. Mheshimiwa Majaliwa alitembelea kiwanda hicho Desemba 14, 2024. kutoka kushoto ni Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel, Makamu Mwenyekiti wa kampuni hiyo Yussuf Ezzi na wa Kwanza kulia ni Makamu Mwenyekiti wa kampuni hiyo Mansoor Moiz (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na Wakazi wa Dege, Wilaya ya Kigamboni Jijini Dar es Salaam leo Desemba 14, 2024 wakati alipokagua utekelezaji wa maagizo ya uwekaji wa taa za Barabarani aliyoyatoa wakati wa ziara yake aliyoifanya wilayani humo Oktoba 2024, ambapo mpaka sasa taa 64 zimeshawekwa na kazi inaendelea (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)