Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais (TAMISEMI) anayeshugulikia Afya Dkt Grace Magembe ametembelea na kukagua huduma zinazotolewa na vituo mbalimbali vya Afya Mkoani Mwanza na kupongeza jitihada kubwa zinazofanywa na watumishi wa Afya.
Amebainisha hayo leo tarehe 21/10/2024 katika ziara ya kukagua utekelezaji wa shughuli za ubora wa huduma katika vituo vya Afya vya Kisesa na Buzuruga vilivyopo jijini Mwanza na kubaini utoaji huduma bora.
“Mnahudumia vizuri mnawajali na mnawapenda na huo ndio uwe muelekeo wetu nimefurahi na nimefarijika sana” Dkt Grace Magembe
“ Mnavyowaona Wananchi wanakuja Kwa wingi na kuwapongeza huduma zinazotolewa ujue ni Kwa namna gani Wananchi wanawaamini” Dkt Grace Magembe
Pia ameongeza kuwa tuendelee kutumia kauli nzuri, lugha nzuri na kumuelimisha mwananchi juu ya huduma zetu hayo yanawezekana Kwa kuwa yako ndani ya uwezo wetu na tuyafanye Kwa uaminifu na kiuadilifu.
Aidha Dkt Grace Magembe amemshukuru Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Dr Jesca Lebba Kwa usimamizi mzuri wa vituo vya Afya na kupunguza malalamiko kutoka Kwa Wananchi.
Katika ziara hiyo Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI anayeshugulikia Afya aliambatana na Wadau kutoa Shirika la Global Fund wanaosaidia Ugonjwa wa kifua kikuu, UkIMWI, Malaria na Mifumo mbalimbali ya Afya.