Featured Kitaifa

MAKAMU WA RAIS AJIANDIKISHA DAFTARI LA WAPIGA KURA BUHIGWE

Written by mzalendoeditor

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango na Mwenza wake Mama Mbonimpaye Mpango wameshiriki zoezi la Uandikishaji kwenye Daftari la Wapiga kura kwaajili ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa katika Kitongoji cha Kihanga Kijiji cha Kasumo Wilaya ya Buhigwe Mkoani Kigoma. Tarehe 12 Oktoba 2024.

……….

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango na Mwenza wake Mama Mbonimpaye Mpango wameshiriki zoezi la Uandikishaji kwenye Daftari la Wapiga kura kwaajili ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa katika Kitongoji cha Kihanga Kijiji cha Kasumo Wilaya ya Buhigwe Mkoani Kigoma leo tarehe 12 Oktoba 2024.

Akizungumza na wanakijiji wa Kasumo mara baada ya kujiandikisha, Makamu wa Rais amesema zoezi la kujiandikisha katika daftari la kupiga kura ni muhimu kwa kuwa ni wajibu kushiriki katika kuchagua viongozi watakaoweza kuwasaidia wananchi. Amesema viongozi wa serikali za mitaa ndiyo wanaoishi jirani zaidi na wananchi hivyo ni muhimu kushiriki katika kuwachagua wale watakaolinda maslahi ya jamii husika.

Makamu wa Rais ameongeza kwamba upatikanaji wa viongozi wazuri unaanza kwa kujiandikisha na baadae kujitokeza kupiga kura hivyo amewasihi kushiriki kikamilifu katika mazoezi yote ya uchaguzi yanayotarajiwa hivi karibuni.

Halikadhalika Makamu wa Rais ametoa wito wa kipekee kwa wanawake kujitokeza katika kugombea nafasi mbalimbali za uongozi kwa kuwa wanazifahamu vema changamoto za jamii na pia wanao uwezo wa kuongoza vizuri.

Amesisitiza wananchi kushiriki vema chaguzi zote kwa amani na utulivu kwa kujiepusha na lugha zisizo na staha pamoja na vurugu wakati wa kampeni.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango na Mwenza wake Mama Mbonimpaye Mpango wameshiriki zoezi la Uandikishaji kwenye Daftari la Wapiga kura kwaajili ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa katika Kitongoji cha Kihanga Kijiji cha Kasumo Wilaya ya Buhigwe Mkoani Kigoma. Tarehe 12 Oktoba 2024.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akizungumza na wanakijiji wa Kasumo mara baada ya kujiandikisha katika Daftari la Wapiga kura kwaajili ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa katika Kitongoji cha Kihanga Kijiji cha Kasumo Wilaya ya Buhigwe Mkoani Kigoma. Tarehe 12 Oktoba 2024.

About the author

mzalendoeditor