Featured Kitaifa

UWT MKOA WA IRINGA WATOA TAMKO KULAANI BAWACHA KUCHOMA MOTO KITENGE CHENYE PICHA YA MWENYEKITI CCM TAIFA

Written by mzalendo

Na Mwandishi Wetu,  Iringa. 

JUMUIYA ya Umoja wa wanawake wa chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Iringa wamelaani vikali kitendo cha Wanawake wa Chadema Bawacha kuchoma moto kitenge chenye picha ya Mwenyekiti wa ccm Taifa Rais Dk.Samia Suluhu Hassan.

Akizungumza na vyombo vya habari katika Ofisi ya CCM mkoa wa Iringa,Mwenyekiti wa jumuiya hiyo mkoa Zainabu Mwamwindi amesema kitendo hicho siyo cha kiungwana na kinaashiria uvunjifu wa amani pia ni niudhalilisha kwa Mhe.Rais.

Zainabu amesema amani ikitoweka nchini kundi kubwa litakaloathirika ni wazee,akina mama na watoto,hivyo Amani tuliyonayo ambayo ni Tunu ya Taifa inapaswa kulindwa na kutetewa na kila mtanzania.
Aidha UWT imewakumbusha BAWACHA msemo wa Mhe,Rais mstaafu wa Serikali ya awamu ya nne Jakaya Mrisho Kikwete usemao’’Akili ya kuambiwa changanya na yako.

“Tunajiuliza hawa BAWACHA ni wanawake wa Tanzania? kwa nini wanapenda kuanzisha chokochoko wakati wanawake wa Tanzania tunapenda sana kulinda amani ya Nchi yetu.Kwa kauli moja UWT mkoa wa Iringa Tunalaani vikali na kukemea kitendo hicho, kisijirudie tena’’Amesema.

Septemba 30 /2024 wanawake wa chama cha Demokrasi na maendeleo Chadema BAWACHA walichoma moto vitenge walivyopewa na Mhe.Rais Dk.Samia Suluhu Hassan vikiwa na picha yake kwenye kongamano la BAWACHA lililofanyika Machi 19,2023 na toleo la kwanza la kitenge hicho lililtolewa Machi 13,2023.

About the author

mzalendo