Featured Kitaifa

EWURA YAELIMISHA WATU WENYE ULEMAVU MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA DAR ES SALAAM

Written by mzalendoeditor

 

Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Mussa Azzan Zungu, akihutubia jumuia ya watu wenye ulemavu wakati wa ufunguzi wa semina kwa kundi hilo maalum kuhusu huduma zitolewazo na EWURA katika sekta ya Nishati na Maji, leo jijini Dar es Salaam. Aliyeketi ni mwenyekiti wa Chama cha Sauti ya wanawake walemavu (VODIWOTA) Bi. Stella Jairos.

Mwenyekiyi wa Chama cha Sauti ya Walemavu Wanawake Tanzania (VODIWOTA) Bi Stella Jairos akizungumzia umuhimu wa semina hiyo kwa wanachama anaowaongoza.

Meneja wa EWURA Kanda ya Mashariki, Mha. Nyirabu Musira akizungumza wakati wa semina kwa watu wenye ulemavu kuhusu umuhimu wa nishati safi ya kupikia jijini Dar es Salaam.

Wanachama wa VODIWOTA na wadau wengine wa masuala ya ulemavu wakiwa kwenye semina ya EWURA kuhusu umuhimu wa matumizi ya nishati safi ya kupikia jijini Dar es Salaam.

….

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) leo 3 Septemba 2024 imewaelimisha wanachama wa jumuia ya watu wenye ulemavu wa jijini Dar es Salaam kuhusu umuhimu wa matumizi ya nishati safi ya kupikia.

Akifungua semina hiyo, Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, Mh. Musa Azzan Zungu, amewasihi wanachama hao kutumia nishati safi ya kupikia ili kujikinga na madhara ya kiafya na kimazingira.

“Nishati safi ya kupikia itaokoa afya zetu na kutunza mazingira yetu,” alisisitiza Mh. Zungu.

Meneja wa EWURA Kanda ya Mashariki, Mha. Nyirabu Musira ameeleza dhima ya EWURA kuelimisha kundi hilo ni kuhakikisha kuwa halibaki nyuma katika matumizi ya nishati safi.

Mwenyekiti wa Chama cha Sauti ya Wanawake Walemavu (VODIWOTA) Bi. Stellah Jairos, ameshukuru EWURA kwa semina hiyo na kwamba anatarajia itawanufaisha sana washiriki katika matumizi ya nishati.

About the author

mzalendoeditor