Timu za mpira wa miguu za Geita DC,Msalala DC,Tanga Jiji na Ifakara TC zimefanikiwa kuinga hatua ya nusu fainali ya michuani ya Shirikisho la Michezo Serikali za Mitaa -SHIMISEMITA inahusisha Halmashauri 100 za Tanzania bara inayoendelea jijini Mwanza.
Katika mchezo huo wa mpira wa miguu timu ya Geita DC imefanikiwa kuitoa Kaliua DC kwa goli 2-0 na kuingia hatua ya nusu fainali, huku Msalala DC ikifanikiwa kuiondosha Tarime TC kwa goli 2-1 na kuingia hatua ya nusu na Tanga Jiji imemtoa Manyoni DC kwa goli 1-0 na kufanikiwa kuingia hatua ya Nusu Fainali.
Halkadhalika Ifakara TC imeitoa Temeke MC kwa goli 2-0 na kutinga Nusu Fainali ,hivyo timu ya Geita DC atakutana na Msalala DC katika uwanja wa Butimba na Ifakara TC itakutana na Tanga Jiji katika uwanja wa Magereza Butimba jijini Mwanza katika hatua ya Nusu Finali
Michezo mingine inayochezwa ni mpira wa Kikapu(Basketball),Pete(Netball),Wavu(Volleyball),mpira wa mikono(handball),Riadha,Kuvuta kamba,Pool table,Draft,Bao,kurusha Vishare,kwaya na ngoma.
Mashinando haya ya SHIMISEMITA yatafungwa tarehe 05.09.2024.