Featured Kitaifa

UDOM YAJA NA UBUNIFU WA KUZALISHA MVINYO UTOKANAO NA ASALI

Written by mzalendo

 

 

Mkurugenzi wa Kitengo Cha Mawasiliano na Masoko chuo kikuu Cha Dodoma (UDOM) Bi.Rose Joseph,akizungumza  kwenye banda la EWURA katika maonesho ya wakulima  Nanenane yanayofanyika katika viwanja vya Nzuguni,jijini Dodoma .

Na.Alex Sonna-DODOMA

KATIKA kuongeza thamani zao la asali nchini Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kimekuja na ubunifu wa kuzalisha mvinyo utokanao na asali.

Hayo yameelezwa leo Agosti 6,2024 na Mkurugenzi wa Kitengo Cha Mawasiliano na Masoko chuo kikuu Cha Dodoma (UDOM) Bi.Rose Joseph,wakati akizungumza na waandishi wa habari   kwenye maonesho ya wakulima kitaifa Nanenane yanayofanyika katika viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma.
Bi.Rose amesema kuwa  pamoja na mambo mengine chuo hicho kimekuwa kikijihisisha na ufugaji nyuki na kuzalisha zao la asali.
“Chuo kikuu cha UDOM katika maonesho haya kimekuja ubunifu wa kutumia zao la asali kuzalisah mvinyo ili kuongeza thamani ya mazao yatokanayo na nyuki”Bi.Rose
Aidha amesema kuwa mazao mengine wanayozalisha yatokanayo na nyuki ni pamoja asali yenye na nta.
Amesema pia UDOM, wamebuni teknolojia y ufugaji samaki ambayo wananchi wanaweza kuitumia kujiongezea kipato na kujikwamua kiuchumi.
” Katika teknolojia hii tumebunifu mfumo ambao unaweza kuutumia kuosha Samaki hata kama hautakuepo eneo husika kwa kuseti muda na chakula kiasi gani unataka walishwe Sasaki kupitia tekonolojia hii”amesema
Amesema ubunifu mwingine ni tekonoloji ya kubainj magonjwa ya mifugo ambayo yamekuwa yakiwakabili wafugaji na kupunguza tija ya mifugo nchini.
“Ubunifu mwingine ni ugugaji wa sunglasses kisasa ambapo mkojo wake unatumika kama viwatilifu kwenye mimea ya bustani lakini kinyesi chao kinatumika kama mbolea hivyo kuondoa matumizi ya kemikali”amesema 
Hata hivyo, ametoa wito kwa Vijana ambao wanasifa kujiunga na kozi mbalimbali ambazo zinatolewa na chuo hichi hivi sasa.
“Dirisha la usajili.lilishafunguliwa tangu mwezi Julai hivyo niwaombe watu wenye sifa kuomba kujiunga na chuo chetu ili wapate ujuzi utakao wasaidi kujiajiri na kuwa chachu katika jamii zao”amesema

About the author

mzalendo