Featured Kitaifa

BALOZI NCHIMBI ATUA KIGOMA, KUTIKISA KANDA YA ZIWA

Written by mzalendoeditor

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi amewasili mkoani Kigoma tayari kuanza ziara ya mikoa mitano ya Kigoma, Geita, Kagera, Mara na Mwanza

Balozi Nchimbi amewasili leo asubuhi Agosti 4, 2024 katika Uwanja wa Ndege wa Kigoma akiwa amembatana na Katibu wa NEC, Oganaizesheni, Ndg. Issa Haji Usi Gavu, Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo Ndg. Amos Makalla, Katibu wa NEC-Organaizesheni, pamoja na Katibu wa NEC – Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Ndg. Rabia Abdallah Hamid.

Baada ya kutua, Katibu Mkuu Balozi Nchimbi pamoja na ujumbe wake amelakiwa na viongozi mbalimbali wa chama na serikali wa mkoa huo,tayari kwa kuanza ziara ya siku 3 mkoani humo.

Malengo ya ziara hiyo ni pamoja na kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020, kuhamasisha uhai wa chama, kusikiliza na kutatua kero za wananchi pamoja na kuhamasisha wananchi kujitokeza kuhakiki taarifa zao na kujiandikisha katika Daftari la Wakaazi kwa ajili ya maandalizi ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Novemba mwaka huu.

About the author

mzalendoeditor