Featured Kitaifa

RAIS SAMIA AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA SHULE YA SEKONDARI YA WASICHANA YA MKOA WA RUKWA

Written by mzalendo

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akivuta kitambaa kuweka jiwe la Msingi la ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mkoa wa Rukwa kwenye hafla iliyofanyika katika Kijiji cha Mtindilo Laela mkoani humo tarehe 17 Julai, 2024.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mkoa wa Rukwa mara baada ya kuweka jiwe la Msingi la ujenzi wa Shule hiyo kwenye hafla iliyofanyika katika Kijiji cha Mtindilo Laela mkoani humo tarehe 17 Julai, 2024.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mkoa wa Rukwa mara baada ya kuweka jiwe la Msingi ujenzi wa Shule hiyo iliyopo Laela Mkoani humo tarehe 17 Julai, 2024.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akimwagilia maji Mti wa Matunda aina ya Parachi mara baada ya kupanda kama kumbukumbu katika viwanja vya Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mkoa wa Rukwa tarehe 17 Julai, 2024.

About the author

mzalendo