Featured Kitaifa

OJADACT, ERC WATOA MAFUNZO YA UANDISHI WA HABARI ZA UCHOKONOZI KWENYE UHALIFU WA MAZINGIRA

Written by mzalendoeditor
Katibu Tawala Wilaya ya Nyamagana Mhe. Yonas Alfred  akifungua Mafunzo ya Uandishi wa Habari za Uchokonozi (Investigative Journalism) kwenye uhalifu  wa masuala ya uhifadhi wa mazingira.
 
Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog

Chama cha Waandishi wa Habari wa Kupiga vita Matumizi ya Dawa za Kulevya na Uhalifu Tanzania (OJADACT) kwa kushirikiana na Shirika la Kimataifa la  Environmental Reporting Collective la Nchini Malaysia (ERC) kimeendesha mafunzo ya siku moja ya  Uandishi wa Habari za Uchokonozi (Investigative Journalism) kwenye Sekta ya  Uhifadhi wa Mazingira kwa waandishi wa Habari Mkoa wa Mwanza.

Mafunzo  hayo ya Uandishi wa Habari za Uchokonozi (Investigative Journalism) kwenye uhalifu  wa masuala ya uhifadhi wa mazingira yamefanyika leo Jumamosi Aprili 2,2022 katika Ukumbi wa Nyakahoja Jijini Mwanza na kukutanisha pamoja waandishi wa habari 20 kutoka Vyombo mbalimbali ya Habari ambapo Mgeni rasmi alikuwa Katibu Tawala Wilaya ya Nyamagana Mhe. Yonas Alfred kwa niaba ya Mkuu wa wilaya hiyo Mhe. Hassan Masala.
Akifungua Mafunzo hayo, kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Katibu Tawala wa Nyamagana Bwana  Yonas Alfred   ameipongeza OJADACT kwa kuandaa mafunzo kwa waandishi wa habari ili waweze kuwa wabobezi wa kuandika habari za uhalibifu wa mazingira na kwamba elimu watakayopata waandishi hao itawasaidia na kuwawezesha kufanya kazi kwa weledi mkubwa.
“Suala la uhifadhi wa mazingira kwa sasa ni Ajenda ya Kidunia. Bila Mazingira viumbe akiwemo binadamu kesho yetu haiwezi kukamilika, hivyo kuandika habari za uhifadhi wa mazingira ni jambo muhimu sana”,amesema.
Amefafanua kuwa Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan inatoa kipaumbele kwenye suala la mazingira ndiyo maana kuna Sera ya Mazingira na Kanuni mbalimbali zinazosisitiza kutunza na kuhifadhi mazingira.
“Kuna mfano wazi kuwa wilaya yetu ya Nyamagana na Mkoa wa Mwanza una changamoto nyingi za kimazingira, kuna uvuvi haramu ndani ya Ziwa Victoria, kuna ukataji hovyo wa miti kwa ajili ya shughuli za uchomaji wa mkaa. Naomba changamoto hizi zote baada ya kupata mafunzo haya maalumu ya kuandika habari za uhifadhi wa mazingira basi nendeni mkafichue uhalibifu huo wa mazingira kwa kutumia kalamu zenu”,ameeleza Alfred.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari wa Kupiga vita Matumizi ya Dawa za Kulevya na Uhalifu Tanzania (OJADACT), Edwin Soko amesema mafunzo hayo yamelenga kuwa mafunzo ya Uandishi wa Habari za Uchokonozi (Investigative Journalism) kwenye Sekta ya Mazingira yamelenga kuwajengea uwezo waandishi wa Habari ili kuhakikisha kuwa wanakuwa wabobezi katika uandishi wa habari za uhalifu wa mazingira ili kuwa na uhifadhi wa Mazingira.
“Leo tumekutana na waandishi wa habari 20 wa mkoa wa Mwanza lakini Aprili 9,2022 tutafanya mafunzo mengine kama haya yatakayoshirikisha waandishi wa habari 20 kutoka mikoa mbalimbali”,amesema Soko.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Katibu Tawala Wilaya ya Nyamagana Mhe. Yonas Alfred  akifungua Mafunzo ya Uandishi wa Habari za Uchokonozi (Investigative Journalism) kwenye uhalifu  wa masuala ya uhifadhi wa mazingira kwa waandishi wa Habari Mkoa wa Mwanza leo Jumamosi Aprili 2,2022 katika Ukumbi wa Nyakahoja Jijini Mwanza. Kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari wa Kupiga vita Matumizi ya Dawa za Kulevya na Uhalifu Tanzania (OJADACT), Edwin Soko, kulia ni Katibu Msaidizi wa OJADACT Isack Wakuganda. Picha na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Katibu Tawala Wilaya ya Nyamagana Mhe. Yonas Alfred  akifungua Mafunzo ya Uandishi wa Habari za Uchokonozi (Investigative Journalism) kwenye uhalifu  wa masuala ya uhifadhi wa mazingira kwa waandishi wa Habari Mkoa wa Mwanza
Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari wa Kupiga vita Matumizi ya Dawa za Kulevya na Uhalifu Tanzania (OJADACT), Edwin Soko akizungumza wakati wa Mafunzo ya Uandishi wa Habari za Uchokonozi (Investigative Journalism) kwenye uhalifu  wa masuala ya uhifadhi wa mazingira kwa waandishi wa Habari Mkoa wa Mwanza.

Mratibu wa Chama cha Waandishi wa Habari wa Kupiga vita Matumizi ya Dawa za Kulevya na Uhalifu Tanzania (OJADACT), Lucyphine Kilanga akiwasilisha mada kuhusu masuala ya uhalifu wakati wa Mafunzo ya Uandishi wa Habari za Uchokonozi (Investigative Journalism) kwenye uhalifu  wa masuala ya uhifadhi wa mazingira kwa waandishi wa Habari Mkoa wa Mwanza.
Katibu wa Chama cha Waandishi wa Habari wa Kupiga vita Matumizi ya Dawa za Kulevya na Uhalifu Tanzania (OJADACT), Martine Nyoni akizungumza wakati wa Mafunzo ya Uandishi wa Habari za Uchokonozi (Investigative Journalism) kwenye uhalifu  wa masuala ya uhifadhi wa mazingira kwa waandishi wa Habari Mkoa wa Mwanza.
Katibu Msaidizi wa Chama cha Waandishi wa Habari wa Kupiga vita Matumizi ya Dawa za Kulevya na Uhalifu Tanzania (OJADACT), Isaack Wakuganda akizungumza wakati wa Mafunzo ya Uandishi wa Habari za Uchokonozi (Investigative Journalism) kwenye uhalifu  wa masuala ya uhifadhi wa mazingira kwa waandishi wa Habari Mkoa wa Mwanza.

Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari wa Kupiga vita Matumizi ya Dawa za Kulevya na Uhalifu Tanzania (OJADACT), Edwin Soko akiwasilisha mada kuhusu Uandishi wa Habari za Uchunguzi kwenye Mafunzo ya Uandishi wa Habari za Uchokonozi (Investigative Journalism) kwenye uhalifu  wa masuala ya uhifadhi wa mazingira kwa waandishi wa Habari Mkoa wa Mwanza.

Waandishi wa habari wakiwa kwenye Mafunzo ya Uandishi wa Habari za Uchokonozi (Investigative Journalism) kwenye uhalifu  wa masuala ya uhifadhi wa mazingira 

Katibu Tawala Wilaya ya Nyamagana Mhe. Yonas Alfred  akipiga picha ya kumbukumbu na Waandishi wa habari walioshiriki Waandishi wa habari wakiwa kwenye Mafunzo ya Uandishi wa Habari za Uchokonozi (Investigative Journalism) kwenye uhalifu  wa masuala ya uhifadhi wa mazingira 
Katibu Tawala Wilaya ya Nyamagana Mhe. Yonas Alfred  akipiga picha ya kumbukumbu na Waandishi wa habari walioshiriki Waandishi wa habari wakiwa kwenye Mafunzo ya Uandishi wa Habari za Uchokonozi (Investigative Journalism) kwenye uhalifu  wa masuala ya uhifadhi wa mazingira.
 
Picha na Kadama Malunde – Malunde 1 blog

About the author

mzalendoeditor