Featured Kitaifa

DK.MWINYI: MAZINGIRA MAZURI YA UWEKEZAJI YAMEIMARISHA SEKTA YA SUKARI

Written by mzalendo
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akihutubia na kuufungua Mkutano wa Wazalishaji wa Sukari katika Nchi SADC, ufunguzi huo uliyofanyika leo 10-7-2024 katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Kiembesamaki Wilaya ya Magharibi “B” Unguja Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu)
Na Mwandishi Wetu
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali ya Tanzania imeweka mazingira mazuri ya uwekezaji ambayo yameleta mafanikio makubwa na kuwezesha kuongezeka kwa uwekezaji mkubwa wa mitaji katika sekta ya sukari.
Aidha, ametoa rai kwa nchi Wanachama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kutumia fursa walizonazo kuweka mazingira bora zaidi ya uwekezaji ili kukuza uwekezaji katika uzalishaji wa sukari.
Akifungua leo Julai 10, 2024 Mkutano wa wazalishaji wa sukari wa nchi za SADC uliofanyika Zanzibar, Dk.Mwinyi amesema mazingira hayo mazuri yamechagiza  viwanda vyote hapa nchini kufanya upanuzi wa kilimo cha miwa na uzalishaji sukari
“Sekta ya sukari ni sekta iliyopewa kipaumbele katika kilimo cha nchi kwa kuwa viwanda vya sukari ni vitovu muhimu vya kilimo na uchumi  Tanzania na pamoja na umuhimu huu, uzalishaji wa sukari kwenye nchi yetu ni moja ya nyenzo kuu na muhimu ya kuimarisha na kulinda usalama wa chakula, kwa kuwa sukari ni moja ya chakula muhimu nchini,”amesema.
Aidha, amesema uzalishaji wasSukari ndani ya Tanzania kama ilivyo kwa nchi nyingine wanachama wa SADC zinazozalisha Sukari, huokoa matumizi ya fedha nyingi za kigeni kila mwaka ambazo zingetumika kuagizia Sukari nje ya nchi, kama Sukari isingezalishwa kwenye nchi.
“Ni dhahiri kuwa, kujenga mazingira bora na kuondoa vikwazo vya uwekezaji katika Sekta ya Sukari kwenye nchi zetu kutawezesha kustawisha zaidi masoko ya ndani ya nchi za SADC na kuongeza fursa ya biashara ya Sukari katika Soko la pamoja la Afrika (AfCFTA) na Dunia kwa ujumla,” amesema.
Amepongeza nchi wanachama wa SADC kupitia utaratibu rasmi wa kuendeleza sekta ya sukari kupitia biashara ya SADC na kusema kuwa serikali itaendelea kuweka na kuboresha mazingira ya uwekezaji ili sekta ya sukari barani Afrika iweze kuwa na ushindani na kuleta manufaa zaidi kwa wananchi.
Pamoja na hayo, Dk.Mwinyi, alisema imani yake mkutano huu utatoa fursa kwa wadau wa sekta ya sukari kubadilishana mawazo na uzoefu kwa lengo la kuimarisha mazingira wezeshi kwa maendeleo endelevu ya Sekta ya Sukari katika nchi wanachama wa SADC na Afrika.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na Mwenyekiti wa Chama cha Wazalishaji Sukari Tanzania (TSPA) Bw.Seif Ali Seif, alipowasili katika viwanja vya Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Kiembesamaki  Wilaya ya Magharibi “B” Unguja Jijini Zanzibar leo 10-7-2024 kwa ajili ya ufunguzi wa Mkutano wa Wazalishaji Sukari wa Nchi za SADC, na (kushoto kwake) Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar Mhe.Omar Said Shaban.(Picha na Ikulu)

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar Mhe.Omar Said Shaban na (kulia kwa Rais) Mwenyekiti wa Chama cha Wazalishaji Sukari Tanzania (TSPA)  Bw. Seif Ali Seif na (kushoto kwa Waziri) Waziri wa Viwanda na Biashara Tanzania Mhe.Dkt. Seleman Jafo, alipowasili katika viwanja vya Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Kiembesamaki  Wilaya ya Magharibi “B” Unguja Jijini Zanzibar leo 10-7-2024 kwa ajili ya ufunguzi wa Mkutano wa Wazalishaji Sukari wa Nchi za SADC.(Picha na Ikulu)

WASHIRIKI wa Mkutano wa Wazalishaji wa Sukari wa Nchi za SADC, wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) akihutubia na kuufungua mkutano huo leo 10-7-2024, uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Kiembesamaki Wilaya ya Magharibi “B” Unguja Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu)

BAADHI ya Wakulima wa Miwa wakifuatilia ufunguzi wa Mkutano wa Wazalishaji wa Sukari wa Nchi za SADC, wakati Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) akihutubia na kuufungua mkutano huo unaofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Kiembesamaji Jijini Zanzibar leo 10-7-2024.(Picha na Ikulu)

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akihutubia na kuufungua Mkutano wa Wazalishaji wa Sukari katika Nchi SADC, ufunguzi huo uliyofanyika leo 10-7-2024 katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Kiembesamaki Wilaya ya Magharibi “B” Unguja Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu)

  

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akikabidhiwa TUZO Maalum na Mwenyekiti wa Chama cha Wazalishaji Sukari Tanzania (TSPA)Bw.Seif Ali Seif, baada ya kuufungua Mkutano wa Wazalishaji wa Sukari kwa Nchi za SADC, unaofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Kiembesamaki Wilaya ya Magharibi “B” Unguja Jijini Zanzibar leo 10-7-20214.(Picha na Ikulu)

About the author

mzalendo