Featured Kitaifa

MAANDALIZI YA SIKU YA KISWAHILI COMORO YAIVA

Written by mzalendo

Balozi wa Tanzania nchini Comoro,Saidi Yakubu amewahimiza wapenzi wa lugha ya Kiswahili nchini Comoro kujitokeza kwa wingi Siku ya Jumapili ili kukienzi Kiswahili katika Hafla Rasmi waliyoandaa kwenye Ukumbi wa Bunge mjini Moroni.

Balozi Yakubu aliwaeleza waandishi wa habari kuwa maandalizi yote ya Maadhimisho hayo yamekamilika ambapo Gavana wa Kisiwa cha Ngazidja yalipo makao makuu ya nchi,Mohamed Mze atakuwa Mgeni Rasmi.

Maadhimisho hayo ya Kiswahili nchini Comoro yatajumuisha burudani za Comoro na Tanzania,Matokeo ya Shindano la Insha na pia kuona vyakula vya Utamaduni wa Kiswahili ambapo wapishi mahsusi toka Tanzania watakuwepo.

Maadhimisho ya Kiswahili nchini Comoro yanatarajiwa kuhudhuriwa na wanafunzi,wataalamu wa Kiswahili na wadau toka mashirika ya Kimataifa.

About the author

mzalendo