Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Augustino Senga Julai 01, 2024 alikagua Mradi wa Ujenzi wa kituo cha kata ya Mbangala kilichopo wilaya ya Songwe ambacho kimejengwa kwa nguvu ya wananchi wa kata hiyo na ujenzi wake bado unaendelea mpaka sasa kituo hicho kimeghalimu kiasi cha shilingi Milioni ishirini na tisa laki saba sabini na sita na mia sita arobaini (29,776,640).
Baada ya ukaguzi huo alizungumza na maofisa, wakaguzi na askari wa vyeo mbalimbali ambapo aliwataka kuendelea kutekeleza majukumu yao ya kazi za Polisi kwa kutoa huduma bora kwa wananchi wanaowahudumia ikiwa ni pamoja na kutekeleza maelekezo ya Tume ya Haki Jinai.