Featured Kitaifa

BUNGE LAIDHINISHA MUSWADA WA SHERIA YA FEDHA WA MWAKA 2024

Written by mzalendo
Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akisoma Muswada wa Sheria ya Fedha wa mwaka 2024, ambao umepitishwa na Bunge baada ya kujadiliwa mara ya pili, bungeni jijini Dodoma. Muswada huo unatarajiwa kufanya marekebisho ya sheria za kodi ili kuwezesha utekelezaji wa kisheria wa Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2024/2025.
Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akiteta jambo na Naibu Waziri wa Fedha Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb), wakati wabunge walipokuwa wakichangia Muswada wa Sheria ya Fedha wa mwaka 2024 ambao uliidhinishwa na Bunge hilo, bungeni jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akiteta jambo na Waziri wa Ardhi Mhe. Jerry Slaa (kulia) na Naibu wake Mhe. Geofrey Pinda (katikati), wakati wabunge walipokuwa wakichangia Muswada wa Sheria ya Fedha wa mwaka 2024 ambao uliidhinishwa na Bunge hilo, bungeni jijini Dodoma.
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akiteta jambo na Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Deogratius Ndejembi na Naibu Wake Mhe. Patrobas Katambi, kabla ya wabunge kuidhinisha Muswada wa Sheria ya Fedha wa mwaka 2024, bungeni jijini Dodoma. 
Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) akiteta jambo na Naibu Waziri Mkuu Mhe. Doto Biteko, Waziri wa Habari, Mhe. Nape Nnauye na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Patrobas Katambi, kabla ya Wabunge kuidhinisha Muswada wa Sheria ya Fedha wa mwaka 2024, bungeni jijini Dodoma. 
Naibu Waziri wa Fedha Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb), akipongezana na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Natu El-maamry Mwamba, mara baada wabunge kupitisha Muswada wa Sheria ya Fedha mwaka 2024 na kuahirishwa rasmi kwa shughuli za bunge jijini Dodoma.. 
Katibu Mkuu wa wizara ya Fedha Dkt. Natu El-maamry Mwamba, akiteta jambo na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge, Dkt. Jimmy Yonazi, mara baada Wabunge kupitisha Muswada wa Sheria ya Fedha mwaka 2024 na kuahirishwa rasmi kwa shughuli za Bunge jijini Dodoma. 
Katibu Mkuu wa wizara ya Fedha Dkt. Natu El-maamry Mwamba akisalimiana na Mbunge wa Nsimbo Mhe. Ana Lupembe, mara baada wabunge kupitisha Muswada wa Sheria ya Fedha mwaka 2024 na kuahirishwa rasmi kwa shughuli za Bunge, jijini Dodoma. 

About the author

mzalendo