Featured Kitaifa

DKT.NDIEGE AZINDUA MFUMO WA TEHAMA WA SCCULT (1992) LTD

Written by mzalendo

MRAJIS  wa Vyama vya Ushirika na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Dkt. Benson Ndiege,akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mfumo wa Tehama wa Sccult (1992) LTD kwa ajili ya Uendeshaji na Utoaji Huduma za Vyama vya Ushirika wa Akiba na Mikopo (SACCOS) hafla iliyofanyika leo Juni 21,2024 jijini Dodoma.

MRAJIS  wa Vyama vya Ushirika na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Dkt. Benson Ndiege,akisisitiza jambo  wakati wa uzinduzi wa Mfumo wa Tehama wa Sccult (1992) LTD kwa ajili ya Uendeshaji na Utoaji Huduma za Vyama vya Ushirika wa Akiba na Mikopo (SACCOS) hafla iliyofanyika leo Juni 21,2024 jijini Dodoma.

NAIBU  Mrajis wa Vyama vya Ushirika – Udhibiti, Collins Nyakunga,,akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mfumo wa Tehama wa Sccult (1992) LTD kwa ajili ya Uendeshaji na Utoaji Huduma za Vyama vya Ushirika wa Akiba na Mikopo (SACCOS) hafla iliyofanyika leo Juni 21,2024 jijini Dodoma.

KATIBU Mtendaji SCCULT (1992) LTD Hassan Mnyone (ADE) ,akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mfumo wa Tehama wa Sccult (1992) LTD kwa ajili ya Uendeshaji na Utoaji Huduma za Vyama vya Ushirika wa Akiba na Mikopo (SACCOS) hafla iliyofanyika leo Juni 21,2024 jijini Dodoma.

BAADHI ya Washiriki wakimsikliza Mrajis wa Vyama vya Ushirika na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Dkt. Benson Ndiege (hayupo pichani), wakati wa uzinduzi wa Mfumo wa Tehama wa Sccult (1992) LTD kwa ajili ya Uendeshaji na Utoaji Huduma za Vyama vya Ushirika wa Akiba na Mikopo (SACCOS) hafla iliyofanyika leo Juni 21,2024 jijini Dodoma.

MRAJIS  wa Vyama vya Ushirika na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Dkt. Benson Ndiege,akipiga makofi mara baada ya kuzindua  Mfumo wa Tehama wa Sccult (1992) LTD kwa ajili ya Uendeshaji na Utoaji Huduma za Vyama vya Ushirika wa Akiba na Mikopo (SACCOS) hafla iliyofanyika leo Juni 21,2024 jijini Dodoma.

MRAJIS  wa Vyama vya Ushirika na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Dkt. Benson Ndiege,akipata maelezo  mara baada ya kuzindua  Mfumo wa Tehama wa Sccult (1992) LTD kwa ajili ya Uendeshaji na Utoaji Huduma za Vyama vya Ushirika wa Akiba na Mikopo (SACCOS) hafla iliyofanyika leo Juni 21,2024 jijini Dodoma.

MRAJIS  wa Vyama vya Ushirika na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Dkt. Benson Ndiege,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuzindua  Mfumo wa Tehama wa Sccult (1992) LTD kwa ajili ya Uendeshaji na Utoaji Huduma za Vyama vya Ushirika wa Akiba na Mikopo (SACCOS) hafla iliyofanyika leo Juni 21,2024 jijini Dodoma.

……………….
MRAJIS  wa Vyama vya Ushirika na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Dkt. Benson Ndiege amevitaka Vyama vya Ushirika wa Akiba na Mikopo (SACCOS) kutumia mifumo ya Kidijitali katika uendeshaji na uchakataji wa taarifa za Wanachama ili kuboresha utendaji na utunzaji wa Taarifa za Kifedha.
Mrajis ametoa kauli hiyo  wakati wa Uzinduzi wa Mfumo wa TEHAMA wa Chama Kikuu cha Ushirika wa Akiba na Mikopo SCCULT (1992) Ltd kwa ajili ya uendeshaji na utoaji huduma za Vyama vya Ushirika wa Akiba na Mikopo (SACCOS) hafla iliyofanyika leo Juni 21, 2024 Jijini Dodoma.
Dkt.Ndiege amesema kuwa utekelezaji wa uendeshaji wa Vyama vya Ushirika kwa kutumia mifumo ya TEHAMA ni sehemu ya maono makubwa ya Serikali ya Serikali ya Awamu ya Sita ambayo inahitaji Vyama vya Ushirika kuwanufaisha Wanachama na kukuza Uchumi.
“Kama ilivyo lengo la Serikali ni kuzitaka SACCOS zote zitumie mfumo wa Tehama ili kunufaisha wanachama na watanzania Kwa ujumla kupitia vyama vya ushirika.”amesema Dkt.Ndiege
Aidha Dkt.Ndiege amekielekeza Chama Kikuu SCCULT kuwa Mfumo wa Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (MUVU) Mfumo unaosimamiwa na Tume ya Maendeleo ya Ushirika (TCDC) kwa lengo la kuhakikisha kuwa Tume inapata taarifa za Vyama kwaajili ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Ushirika.
Hivyo, TEHAMA kutumika kama chachu ya kuongeza tija, uwazi na kasi ya uchumi.
Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Ushirika Kolimba Tawa amesema Mfumo huo unaenda kutatua changamoto ya upatikanaji wa Taarifa za Vyama.
“Mfumo huu utaongeza uwazi na uwajibikaji kutokana na taarifa kuchakatwa na zaidi ya mhusika mmoja, kutengeneza ripoti zinazohitajika na wadau kwa wakati pamoja na upatikanaji wa  kumbukumbu hasa  panapojitokeza changamoto.”amesema
Mfumo huo wa TEHAMA wa Chama Kikuu cha Ushirika wa Akiba na Mikopo SCCULT (1992) Ltd umeundwa kwa kushirikisha Kampuni ya UBX, Umoja Switch, DSIK pamoja na Vyama mbalimbali vya Ushirika wa Akiba na Mikopo (SACCOS).

About the author

mzalendo