Leo Juni 12, 2024 Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) imekutana na Kufanya mazungumzo na Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Dkt John Mboya.
Ujumbe wa THBUB uliongozwa na Mhe.Mohamed Khamis Hamad, Makamu Mwenyekiti wa THBUB. Katika ziara hiyo Mhe. Mohamed aliambatana na Mkurugenzi Msaidizi na Maafisa wa THBUB.
Mhe.Mohamed alieleza kuwa lengo la ziara ya THBUB Mkoani Tabora ni kutoa elimu kwa umma kuhusu masuala ya Haki za Binadamu na Misingi ya Utawala Bora pamoja na kusikiliza malalamiko ya wananchi kuhusu uvunjwaji wa haki za binadamu na ukiukwaji misingi ya utawala bora, kutembelea na kukagua Gereza Kuu Uyui na Kituo cha Polisi Uyui.
Kwa upande wake Katibu Tawala Dkt.Mboya ameipongeza THBUB kwa kufika Mkoani hapo, kusikiliza Wananchi na kutoa elimu.
Aidha Dkt. Mboya alitoa wito kwa THBUB kufungua Ofisi Mikoani ili wananchi waweze kupata huduma kwa ukaribu zaidi.
Ziara ya THBUB Mkoani Tabora itafanyika kwa Muda wa Siku Sita na inatarajia kutoa elimu kwa Watendaji wa Mitaa, Watendaji wa Kata,Watendaji wa Vijiji na kufanya mikutano ya hadhara kwa Wananchi.