Featured Kimataifa

HUENDA TAIFA LA MEXICO LIKAONGOZWA NA RAIS MWANAMKE KWA MARA YA KWANZA

Written by mzalendo

Hesabu isiyokuwa rasmi iliyotolewa mapema hii leo Jumatatu inaonyesha kwamba mgombea wa chama kinachotawala nchini Mexico Claudia Sheinbaum, anaelekea kushinda uchaguzi mkuu wa urais na kuwa mwanamke wa kwanza kuwa rais wa nchi hiyo.

Mkuu wa taasisi ya uchaguzi ya kitaifa amesema kuwa hesabu hiyo inaonyesha kwamba Sheinbaum, ambaye ni meya wa zamani wa mji wa Mexico, anaelekea kupata ushindi wa kati ya asilimia 58.3 na 60.7 ya kura zilizopigwa.

Mshindani wake mkuu, Xochitl Galvez, ambaye ni seneta kutoka vyama vya upinzani na mfanyabiashara, ana kati ya asilimia 26.6 na 28.6.

Mgombea wa mrengi wa kati Jorge Alvarez Maynez ana kati ya asilimia 9.9 na 10.8.

Hesabu pia inaonyesha kwamba chama chake Sheinbaum kinaelekea kupata idadi kubwa ya viti katika baraza la Congress.

cc Voaswahili.

About the author

mzalendo