Featured Kitaifa

VIONGOZI WA DINI TOENI MAFUNZO KWA WANANDOA NA VIJANA KUWAANDAA KUBEBA MAJUKUMU YA NDOA

Written by mzalendoeditor

 

Na Gideon Gregory, Dodoma.

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima
ametoa wito kwa viongozi wa dini zote kuendelea
kutoa mafunzo kwa wanandoa wanaofunga ndoa
na kwa vijana kupitia mikusanyiko ya vijana
katika madhehebu yao, ili kuwaandaa kubeba
majukumu ya ndoa na kujiandaa kwa
majukumu hayo kabla ya kuingia katika ndoa.

Waziri Dkt. Gwajima ametoa wito huo leo Mei 17,2024 Bungeni Jijini Dodoma wakati akiwasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara yake kwa mwaka wa fedha 2024/25.

Aidha, amesema katika kuelekea mwaka wa fedha 2024/25 Serikali imetenga kiasi cha Shilingi Bilioni 10.5 kwa ajili ya kutoa mikopo yenye masharti nafuu kwa Makundi Maalum hususani wafanyabiashara ndogondogo wakiwemo machinga, mama/baba lishe, waendesha bodaboda na bajaji na ma makundi mengine yenye biashara ndogo halali zilizosajiliwa, ili kuongeza mitaji na kuboresha shughuli zao za kiuchumi.

“katika kutekeleza vipaumbele vilivyoainishwa, Wizara kwa mwaka 2024/25 imekadiria kutumia kiasi cha Shilingi 67,905,259,000, kati ya fedha hizo, Shilingi 47,487,079,000 ni fedha za matumizi ya kawaida ambapo Shilingi 21,650,426,000 ni Fedha za Mishahara na Shillingi 25,836,653,000 ni fedha za uendeshaji wa ofisi, aidha, Shilingi.
20,418,180,000 ni fedha za utekelezaji wa miradi
ya maendeleo ambapo kati ya fedha hizo Shillingi
18,025,673,000 ni fedha za ndani na Shillingi
2,392.507,000 ni fedha za nje”,amesema.

Aidha, ameongeza kuwa kwenye eneo la huduma za ustawi wa jamii na watoto, kiasi cha Shilingi Bilioni 1.2kimetengwa kwa ajili ya kuwezesha utoaji wa huduma za marekebisho ya tabia kwa watoto waliokinzana na sheria, kufuatilia utoaji wa
huduma katika Makao ya Watoto, Vituo vya
Kulelea Watoto wadogo Mchana na Watoto
Wachanga, Kukarabati Shule ya Maadilisho
ya Upanga na Mtwara, na Kuendeleza ujenzi
wa Mahabusu ya Watoto Mwanza.

Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum imeliomba Bunge kwa mwaka wa fedha 2024/25 liidhinishe jumla Shilingi Bilioni 67.9 ili kutekeleza majukumu yake kwa maendeleo na ustawi wa jamii.

About the author

mzalendoeditor