Naibu
Waziri wa Mambo na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Mbarouk
Nassor Mbarouk (Mb) akifungua Mkutano wa Nne wa Baraza la Wafanyakazi la
Wizara lililofanyika katika Ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa
cha Arusha (AICC) tarehe 02 Mei, 2024
………………
Naibu Waziri Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk amefungua Mkutano
wa Nne wa Baraza la Wafanyakazi la Wizara uliofanyika jijini Arusha.
Akifungua Mkutano huo, Mhe. Balozi
Mbarouk amewasihi Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Afrika Mashariki kuendelea kubuni maeneo ya kimkakati ya ushirikiano ambayo
yatakuza na kuendeleza ushawishi wa Tanzania katika majukwaa ya Kikanda na
Kimataifa.
“Nichukue fursa hii kuwasihi
kuendelea kufanya kazi kwa kuzingatia weledi na ubunifu, muendelee kubuni
maeneo ya kimkakati ya ushirikiano ili kuimarisha uhusiano wa uwili, kikanda na
Kimataifa kuendeleza ushawishi wa Tanzania katika majukwaa ya kimataifa,”
alisisitiza Balozi Mbarouk.
Amesema Wizara inaandelea na kazi ya
uandaaji wa Mkakati wa Kitaifa wa utekelezaji wa Diplomasia ya Uchumi
ambao kukamilika kwake kutachochea ufanisi na kuleta tija katika kukuza
Ushirikiano wa kiuchumi na kijamii katika ngazi ya uwili, kikanda na
kimataifa.
Amewataka wafanyakazi wa Wizara
kuimarisha ushirikiano, uhusiano na maelewano miongoni mwao huku wakiendelea
kufanya kazi kwa weledi, ujuzi wa hali ya juu ili kuleta tija na ufanisi kwa
taifa.
Pia amewapongeza wajumbe wa Baraza
kwa kazi nzuri ya kuwawakilisha wafanyakazi wengine katika Baraza hilo.
Awali akizungumza kwenye mkutano huo,
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ambaye
pia ni Mwenyekiti wa Baraza hilo, Balozi Dkt. Samwel Shelukindo amesema Wizara
itaendelea kushughulikia changamoto mbalimbali za Wafanyakazi na kuboresha
mazingira ya kazi ili kuhakikisha utekelezaji wa majukumu ya Wizara unakamilishwa kwa tija na
ufanisi.
Naye Mwenyekiti wa TUGHE Tawi la
Wizara, Bi Pili Sukwa ameawaasa Watumishi wa Wizara kuendelea kutii sheria,
kanuni taratibu na maelekezo mbalimbali yanayotolewa na Viongozi wa
Wizara na Serikali kwa ujumla ili kwa pamoja kufikia malengo tarajiwa.
Mkutano huo, pamoja na mambo mengine
umepokea taarifa mbalimbali za utekelezaji wa majukumu ya Wizara pamoja na
kupokea na kujadili Bajeti ya Wizara kwa mwaka wa fedha 2024/2025 kabla ya
kuwasilishwa kwenye Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Baadhi ya Wajumbe wa Mkutano wa Nne wa Baraza la Wafanyakazi la Wizara wakifuatilia mkutano huo katika Ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) tarehe 02 Mei, 2024 |
Baadhi ya Wajumbe wa Mkutano wa Nne wa Baraza la Wafanyakazi la Wizara wakifuatilia mkutano huo katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) tarehe 02 Mei 2024 |
Baadhi ya Wajumbe wa Mkutano wa Nne wa Baraza la Wafanyakazi la Wizara wakifuatilia mkutano huo katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) tarehe 02 Mei, 2024 |
Meza Kuu wakifuatilia Mkutano wa Nne wa Baraza la Wafanyakazi la Wizara wakifuatilia mkutano huo katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) tarehe 02 Mei, 2024 |
Baadhi ya Wajumbe wa Mkutano wa Nne wa Baraza la Wafanyakazi la Wizara wakifuatilia mkutano huo katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) tarehe 02 Mei, 2024 |