Featured Kitaifa

BILIONI 3.8 KUIMARISHA UTOAJI WA HUDUMA HOSPITALI YA MKOA GEITA

Written by mzalendoeditor

Serikali imepeleka vifaa tiba vyenye thamani ya shilingi bilioni 3.8 kwa ajili ya kuimarisha utoaji wa huduma za Afya katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Geita.

Hayo yamebainishwa na Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel leo Aprili 29, 2024 Jijini Dodoma wakati akijibu swali Namba 198 kutoka kwa Mbunge wa Viti Maalum Mhe. Josephine Tabitha Chagula aliyeuliza Je, lini Serikali itapeleka Watumishi pamoja na Vifaa Tiba katika Hospitaliya Mkoa wa Geita.

Dkt. Mollel amesema Hospitali ya Mkoa Geita ina jumla ya watumishi 349 na katika mwaka wa fedha 2023/2024 Serikali imepeleka watumishi 22 wa kada mbalimbali katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Geita ili kuendelea kuimarisha utaoji wa huduma za afya katika Hospitali hiyo.

About the author

mzalendoeditor