Featured Kitaifa

NDEJEMBI AKUTANA NA NAIBU WAZIRI WA SWEDEN

Written by mzalendo

NAIBU Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhe Deogratius Ndejembi amekutana na kufanya mazungumzo na Naibu Waziri wa Biashara ma Maendeleo ya Kimataifa wa Sweden, Mhe Diana Janse katika Ofisi za Wizara jijini Dodoma leo.

Mazungumzo hayo yalilenga kujadili kuhusiana na kuendeleza ushirikiano wa miaka 60 uliopo baina ya mataifa hayo mawili hasa katika uendelezaji na uboreshaji wa utoaji huduma ya usafiri wa mabasi yaendayo kasi katika Jiji la Dar es Salaam.

Wengine walioshiriki kikao hicho ni Balozi wa Sweden nchini, Mhe Charlotta Ozaki Macias, Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji wa Miundombinu Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhandisi Gilbert Moga na Mkurugenzi wa Fedha kutoka DART, Deusdelity Casmir.

About the author

mzalendo