Kitaifa

CDC TANZANIA KUSHIRIKIANA NA MUHIMBILI KUKABILIANA NA MAGONJWA MBALIMBALI

Written by mzalendo

Mkurugenzi Mkazi wa Kituo cha Kuzuia na Kudhibiti Magonjwa Nchini Marekani (CDC) Tanzania, Dkt. Mahesh Swaminathan amesema kituo hicho kipo tayari kushirikiana na Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) katika kukabiliana na magonjwa mbalimbali yakiwemo ya kuambukiza na yasiyoambukiza.

Dkt. Swaminathan aliyasema hayo jana jioni alipotembelea MNH na kukutana na Uongozi ili kuangalia fursa mbalimbali za ushirikiano kati ya kituo hicho na Hospitali ya Taifa Muhimbili yenye dhamana kubwa katika masuala ya utoaji huduma za kibingwa na ubingwa bobezi, utafiti na elimu kwa ujumla wake kutokana na kuwa hospitali yenye hadhi ya Chuo Kikuu kwenye masuala ya mafunzo. 

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa MNH Prof. Mohamed Janabi amesema hospitali ipo tayari kushirikiana na CDC Tanzania kutokana na hospitali hiyo kuwa na mifumo madhubuti ya kukusanya taarifa, uwepo wa maabara kubwa yenye vifaa vya kisasa vya kufanya uchunguzi na kufanya tafiti mbalimbali.

About the author

mzalendo