Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Bi. Mary Maganga (wa tatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na akina mama wa kikundi cha utunzaji mazingira katika Kijiji cha Magubike, Halmashauri ya Iringa Vijijini wakati wa ziara yake ya kukagua shughuli za hifadhi ya mazingira kupitia Mradi wa Urejeshwaji Endelevu wa Mazingira na Hifadhi ya Bioanuai (SLR) katika Kijiji hicho Februari 28, 2024.
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Bi. Mary Maganga (wa pili kulia) akiwaongoza wajumbe wa Kamati ya Kitaifa ya Usimamizi wa Mradi wa Urejeshwaji Endelevu wa Mazingira na Hifadhi ya Bioanuai (SLR) kwenye ziara ya ukaguzi wa shughuli za utekelezaji wa Mradi huo katika Vijiji vya Ilalasimba na Migubike vilivyopo Halmashauri ya Iringa Vijijini, Februari 28, 2024. Kulia kwake ni Katibu Tawala Mkoa wa Katavi Bw. Rodrick Mpogolo.
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Bi. Mary Maganga (wa pili kulia) akifurahia jambo pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa, Bw. Bashir Muhoja (kushoto), Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa, Mhe. Stephen Mhapa (kulia) na Mratibu wa Kitaifa wa Mradi wa Urejeshwaji Endelevu wa Mazingira na Hifadhi ya Bioanuai (SLR), Dkt. Damas Mapunda (wa pili kushoto) wakati wa ziara ya kukagua Mradi wa Hifadhi ya Msitu wa Kijiji cha Ilalasimba Halmashauri ya Iringa Vijijini Februari 28, 2024
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Bi. Mary Maganga akisoma bango linaloonesha taarifa ya utekelezaji wa Mradi wa hifadhi ya msitu wa Kijiji cha Ilalasimba kilichopo Halmashauri ya Iringa Vijijini wakati wa ziara yake ya kukagua shughuli za hifadhi ya mazingira kupitia Mradi wa Urejeshwaji Endelevu wa Mazingira na Hifadhi ya Bioanuai (SLR) Februari 28, 2024. Mbele yake ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Iringa Vijijini, Bw. Stephen Mhapa.
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Bi. Mary Maganga akitazama moja ya matunda ya asili yanayopatikana katika hifadhi ya msitu wa Kijiji cha Ilalasimba kilichopo Halmashauri ya Iringa Vijijini wakati wa ziara yake ya kukagua shughuli za hifadhi ya mazingira kupitia Mradi wa Urejeshwaji Endelevu wa Mazingira na Hifadhi ya Bioanuai (SLR) Februari 28, 2024. Kushoto ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Iringa Vijijini, Bw. Stephen Mhapa.
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Bi. Mary Maganga akitazama moja ya matunda ya asili yanayopatikana katika hifadhi ya msitu wa Kijiji cha Ilalasimba kilichopo Halmashauri ya Iiringa Vijijini wakati wa ziara yake ya kukagua shughuli za hifadhi ya mazingira kupitia Mradi wa Urejeshwaji Endelevu wa Mazingira na Hifadhi ya Bioanuai (SLR) Februari 28, 2024. Kushoto ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Iringa Vijijini, Bw. Stephen Mhapa.
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Bi. Mary Maganga (katikati) akitazama bango linaloonesha taarifa ya utekelezaji wa Mradi wa shamba darasa la kilimo katika Kijiji cha Ilalasimba kilichopo Halmashauri ya Iringa Vijijini wakati wa ziara yake ya kukagua shughuli za hifadhi ya mazingira kupitia Mradi wa Urejeshwaji Endelevu wa Mazingira na Hifadhi ya Bioanuai (SLR) Februari 28, 2024. Kushoto ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Iringa Vijijini, Bw. Bashir Muhoja na Mratibu wa Mradi wa Urejeshwaji Endelevu wa Mazingira na Hifadhi ya Bioanuai (SLR), Dkt. Damas Mapunda.
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Bi. Mary Maganga (wa tatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na wanakikundi wa kikundi cha Israel kinachojishughulisha na kilimo cha Shamba darasa la Kilimo cha mahindi wakati wa ziara yake ya kukagua shughuli za hifadhi ya mazingira kupitia Mradi wa Urejeshwaji Endelevu wa Mazingira na Hifadhi ya Bioanuai (SLR) Februari 28, 2024. Kulia kwake ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Iringa Vijijini, Bw. Stephen Mhapa.
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Bi. Mary Maganga (wa pili kulia) akipata maelezo kutoka Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Iringa Vijijini, Bw. Bashir Muhoja kuhusu kilimo cha nyasi bora za malisho ya ng’ombe wakati wa ziara yake ya kukagua shughuli za hifadhi ya mazingira kupitia Mradi wa Urejeshwaji Endelevu wa Mazingira na Hifadhi ya Bioanuai (SLR) katika Kijiji cha Ilalasimba kilichopo Wilayani humo Februari 28, 2024. Kulia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Iringa Vijijini, Mhe. Stephen Mhapa.
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Bi. Mary Maganga (kulia) akiongozana na Katibu Tawala Mkoa wa Katavi Bw. Rodrick Mpogolo (katikati) wakati wa ziara ya kukagua shughuli za hifadhi ya mazingira kupitia Mradi wa Urejeshwaji Endelevu wa Mazingira na Hifadhi ya Bioanuai (SLR) katika Kijiji cha Ilalasimba kilichopo Halmashauri ya Iringa Vijijini Februari 28, 2024.
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Bi. Mary Maganga (wa pili kulia nyuma) akiwa katika picha ya pamoja na wanakikundi wanaojishughulisha na ufugaji wa ng’ombe wa maziwa wa kikundi cha Agape kilichopo Kijiji cha Ilalasimba Halmashauri ya Iringa Vijijini wakati wa ziara yake ya kukagua shughuli za hifadhi ya mazingira kupitia Mradi wa Urejeshwaji Endelevu wa Mazingira na Hifadhi ya Bioanuai (SLR) katika Kijiji hicho Februari 28, 2024.
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Bi. Mary Maganga (wa tatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na akina mama wa kikundi cha utunzaji mazingira katika Kijiji cha Magubike, Halmashauri ya Iringa Vijijini wakati wa ziara yake ya kukagua shughuli za hifadhi ya mazingira kupitia Mradi wa Urejeshwaji Endelevu wa Mazingira na Hifadhi ya Bioanuai (SLR) katika Kijiji hicho Februari 28, 2024.
(NA MPIGAPICHA WETU)
Na Mwandishi Wetu,OMR- IRINGA,
KATIBU Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Bi. Mary Maganga amewataka wananchi wa Vijiji vya Magubike na Ilalasimba vilivyopo Kata ya Nzihi Halmashauri ya Iringa Vijijini, Mkoani kufanya shughuli zisizoharibu mazingira ili kutunza uoto wa asili wa maeneo hayo.
Bi. Maganga ameyasema hayo Februari 28, 2024 wakati alipoongoza Ujumbe wa Kamati ya Kitaifa ya Usimamizi wa Mradi wa Urejeshwaji Endelevu wa Mazingira na Hifadhi ya Bioanuai (SLR) kukagua shughuli za utekelezaji wa Mradi katika Kata ya Nzihi, Halmashauri ya Iringa Vijijini, Mkoani Iringa.
Katibu Mkuu Bi. Maganga ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya Usimamizi wa Mradi wa SLR, alikagua shughuli za hifadhi wa mazingira katika Kata hiyo ikiwemo hifadhi ya msitu wa Kijiji cha Ilalasimba, Shamba darasa la kilimo hifadhi, shamba darasa la malisho Kijiji cha Ilalasimba, shughuli za ufugaji ng’ombe wa maziwa na hifadhi ya Kijiji cha Magubike.
Amesema kwa kutambua umuhimu wa uoto wa asili katika maeneo yote ya Mradi, Serikali kupitia Mradi wa SLR imeunda timu ya Wataalamu kutoka Wizara za Kisekta zikiwemo Ofisi ya Rais TAMISEMI, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Wizara ya Maji ikiwa ni mkakati mahsusi wa kurudisha uoto wa asili uliopotea katika maeneo mbalimbali nchini.
“Kwa sisi wa zamani sote ni mashahidi tunakumbuka hali ya maeneo haya ilivyokuwa na uoto wake wa asili tofauti na hali ilivyo sasa…..Ili kurejesha uoto wa asili wa eneo hili tumeleta Mradi huu wa SLR na matunda yameanza kuonekana sasa, tunataka mradi huu uwe wa mfano tusimulie hadithi nzuri kwa vizazi vyetu” Amesema Katibu Mkuu Maganga.
Aidha ameipongeza Timu ya Watalaamu wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa kuongeza kasi ya utoaji wa elimu ya utunzaji wa mazingira kwa wananchi ikiwemo upandaji wa miti kwa mujibu wa maelekezo ya Serikal ili kuepusha athari za mabadiliko ya tabianchi.
Katibu Mkuu Bi. Maganga amesema kuwa ni muhimu shughuli za kilimo, mifugo na misitu ziende sambamba na juhudi za hifadhi ya mazingira ili kuhakikisha mradi huo unakuwa endelevu na hivyo kuendelea kutunza uoto wa asili wa maeneo hayo.
Aidha ameridhishwa na mwamko wa wananchi katika utekelezaji wa miradi ya mazingira, hatua iliyotokana na jamii hizo kuwa mstari wa mbele kusimamia miradi katika kujikwamua kiuchumi na hivyo kuongeza pato la familia.
Amefafanua kuwa uoto wa asili sambamba na upandaji wa miti pia unahusisha utumiaji wa rasilimali zilizopo kwa njia endelevu ikiwa ni pamoja na kuacha maeneo yaliyoharibika kurejesha yenyewe uoto wake wa asili na kuachana na shughuli zinazopelekea uharibifu ikiwemo ukataji miti.
Awali akitoa taarifa ya utekelezaji wa mradi wa SLR, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Bw. Bashir Muhoja amesema Mradi huo unatakelezwa katika Kata tatu ambazo ni Nzihi, Izazi na Migoli pamoja na vijiji nane (8) ambapo kufikia Desemba 2023 Ofisi yake iliidhinishiwa kiasi cha Shilingi Milioni 426 kwa ajili ya utekelezaji wa mradi.
Amebainisha kuwa shughuli zilizotekelezwa ni pamoja na kukamilika kwa ujenzi wa josho na kibanio katika Kijiji cha Makuka, kuwezesha vikundi vinne vya kijamii kutekeleza shughuli mbadala za ufugaji wa ng’ombe wa maziwa, mbuzi na nyuki pamoja na kuwezesha upandaji miti na kuanzisha mashamba darasa ya kilimo na mifugo.
“Hadi kufikia Desemba, 2023 kiasi cha Shilingi Milioni 320.6 zilizopokelewa ambazo ni sawa na asilimia 75.19 na utekelezaji wa shughuli kwa fedha za mwaka 2023 bado unaendelea. Shughuli zinazoendelea kutekelezwa ni pamoja na kusambaza mtandao wa maji kwa wananchi wa Kata ya Migoli na miradi mingine ya maendeleo” amesema Muhoja.
Kwa upande wake, Mratibu wa Kitaifa wa Mradi wa SLR, Dkt. Damas Mapunda Kwa mujibu wa Dkt. Mapunda mradi huo ulianzishwa mahsusi ikiwa ni juhudi za pamoja baina ya Serikali na Wadau wa Maendeleo kukabiliana na athari za uharibifu wa mazingira na mabadiliko ya tabianchi kunakosababishwa na shughuli za kibinadamu ukataji miti, uchomaji mkaa na uharibifu wa vyanzo vya maji.
Ameongeza kuwa Mradi huo pia umekusudia kuandaa mpango wa matumizi bora ya ardhi ili kuwezesha uboreshaji wa ardhi kwa ajili ya kilimo pamoja na malisho ya mifugo ili kuzuia muingiliano wa shughuli za kijamii na kiuchumi katika maeneo yaliyohifadhiwa ikiwemo vyanzo vya maji.
Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa, Bw. Stephen Mhapa ameishukuru Serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais kwa ufadhili wa miradi wa mazingira ambayo imebadili hali ya maisha ya kiuchumi kwa wananchi wake na kuongeza kuwa halmashauri hiyo itahakikisha miradi hiyo inakuwa endelevu.
“Tunachoahidi kwako Katibu Mkuu ni kuhakikisha mradi huu unakuwa endelevu kwa kwa manufaa ya vizazi vijavyo ili wawe mashuhuda wa jitihada za hifadhi ya mazingira zilivyofanywa kwa ustadi mkubwa na jamii zilizopo katika Vijiji vya Ilalasimba na Magubike” amesema Mhapa.
Mradi wa SLR unafadhiliwa na Mfuko wa Mazingira wa Dunia (GEF) kupitia Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP) na kusimamiwa na Ofisi ya Makamu wa Rais ambapo kiasi cha Bilioni 25.8 kimetengwa kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huo.
Mradi wa SLR unatekelezwa kwa kipindi cha miaka mitano kuanzia mwaka 2021 hadi 2025 kukamilika mwaka 2025 ambapo jumla ya Mikoa 5, Halmashauri 7, Kata 18 na vijiji 54 vinanufaika na mradi huo.
Halmashauri zinazonufaika na mradi huo ni Halmashauri ya Iringa Vijijini (Iringa), Wilaya ya Mbeya na Mbarali (Mbeya), Halmashauri za Sumbawanga vijijini (Rukwa) pamoja na Halmashauri za Wilaya za Tanganyika na Mpimbwe (Katavi).