Featured Kitaifa

MAJARIBIO MTAMBO NO. 9 BWAWA LA NYERERE WAFANIKIWA

Written by mzalendoeditor

Mtambo wa kwanza wa kuzalisha umeme katika Bwawa la Mwalimu Nyerere umefanikiwa kuwashwa kwa majaribio hali itakayoboresha upatikanaji wa umeme nchini.

Hayo yamebainishwa na leo Februari 16 Bungeni Mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga wakati akijibu swali la Mbunge wa Luepmbe, Edwin Swalle aliyetaka kujua lini Mitambo katika Bwawa hilo itaanza kuwashwa.

“Mwezi wa 6 mwaka huu ndio tulikuwa tumepanga kuwasha Mtambo Namba 9 kwa mara ya kwanza. Lakini kwa jitihada za Serikali na Mkandarasi tuliweza kusogeza ratiba za kuwasha mtambo Namba 9 mpaka mwezi huu wa Pili.

Mhe. Spika naomba kulitaarifu Bunge lako tukufu, jana Februari 15 tumefanikiwa kufanya majaribio kwa ukamilifu kwa Mtambo Namba 9 na tumeutembeza kwa uwezo wake wa mwisho yani Megawati 235,” amesema Naibu Waziri Kapinga.

Naibu Waziri Kapinga pia amewashukuru Watanzania kwa kuendelea kuwavumilia na kuahidi kuwa mtambo huo utazinduliwa mwezi huu na mtambo Namba 8 nao utaanza kuzalisha umeme na kusisitiza kuwa ratiba hiyo iko palepale.

About the author

mzalendoeditor