Featured Kitaifa

TAASISI YA MCCCO KUPANDA MITI MILIONI MOJA KILA MWAKA DODOMA

Written by mzalendo

Na Paul Mabeja, CHAMWINO

TAASISI isiyokuwa ya kiserikali inayojihusisha na mapamabano dhidi ya athari za mabadiliko tabianchi na uhifadhi wa mazingira The Climate Change Conservation Organization (MCCCO) imeweka malengo ya kupanda miti milioni moja kila mwaka mkoani Dodoma ili kuunga mkoa jitihada za serikali kulinda mazingira.

Katibu wa Taasisi hiyo Benard James, akizungumza wakati wa zoezi la upandaji katika shule ya msingi Mlebe alisema wamepanga kila mwaka kupanda miti milioni moja katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa Dodoma ili kuunga mkono jitihada za serikali kulinda mazingira.

“Leo hapa tumeleta miti 2,500 ambayo imepandwa katika eneo la shule ya msingi Mlebe na Zahanati lakini zoezi hili litakuwa endelevu ili kuendeleza mapambano dhidi ya athari za mabadiliko tabianchi”alisema

Mbunge wa viti maalum Riziki Lulida, akiongoza upandaji miti hiyo 2,500 alisema hivi sasa Dunia inakabiliwa na athari za mabadiliko tabianchi ambazo zinatokana na watu kuharibu mazingira kutokana na shunghuli mbalimbali za kibinadamu ikiwemo ukati miti kwa ajili ya kubi na mkaa.

“Niwaombe Watanzania kuachana na matumizi ya nishati ya mkaa kwa ajili ya kupikia na kutumia nishati mbadala ili kutunza mazingira hali ambayo itasadia kurudisha uoto wa asili na kupunguza ukame ulipo katika baaadhi ya mikoa.

“Ukiwa kwenye ndege juu mkoa wa Dodoma unaonekana ni jangwa sana na hii yote ni kutokana ukataji miti ovyo ambao umeharibu mazingira hivyo basi niwaombe wananchi kuacha kukataa miti ovyo kwa ajili ya kuni na mkaa”alisema Lulida

Alisema jitihada za haraka zinahitajika kwenye mikoa ambayo hivi sasa inaonekana kuwa jagwa kutokana na watu kuharibu mazingira.

“Hivi sasa mikoa kama Dodoma,Singida na Arusha ukiwa kwenye ndege juu unaona maeneo hayo ni jangwa kabisa hivyo jitiha da upanadaji miti na kuitunza zinahitajika ili kuunga mkono juhudi za serikali za mapambano dhidi ya athari za mabadiliko tabianchi”alisema

Aidha, alisema katika kubabilina natatizo hilo atangoza taasisi hiyo kupanda miti shule zote za mkoa wa Dodoma ili kuunga mkono juhudi za Rais Samia Suluhu Hassan za kutunza mazingira tangu akiwa Makamu wa Rais mwaka 2017.

About the author

mzalendo