Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Judith Kapinga(katikati) akitembelea na kukagua Miundombinu ya Upakuaji wa Mafuta ya aina yote yanayoingia na kutoka nchini wakati wa ziara yake ya kikazi katika Wakala huo, Jijini Dar es salaam.
Na.Mwandishi Wetu-Dar Es Salaam
Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Judith Kapinga amekagua Maendeleo ya Ujenzi wa Miundombinu ya Kupimia Mafuta yanayoingia na kutoka nchini Pamoja na Ujenzi wa Mapipa mapya ya Kuhifadhi Mafuta Bandarini.
Mhe. Kapinga amefanya ziara hiyo Tarehe 9, Januari 2024, ikiwa ni kufuatilia maelekezo ya Mhe. Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati aliyoyatoa mwishoni mwa Mwezi Oktoba, 2023 alipotembelea Wakala huo na kuagiza kuwa Ujenzi wa Miundombinu Mipya ya kupimia Mafuta yanayoingia na kutoka nchini (Flow Meter) ikamilike kwa wakati na isiathiri utendaji kazi.
Flow Meter inamilikiwa na Serikali kwa asilimia 100 na Mapipa hayo mapya yanamilikiwa na Serikali kwa Asilima 50 kupitia Kampuni yake ya Uhifadhi wa Mafuta TIPER Pamoja na Kampuni ya Orxy kwa Asilima 50 na yana uwezo wa kuhifadhi Lita za Ujazo Milioni 60.
Mara baada yakuona maendeleo ya Ujenzi huo, Mhe. Kapinga amesema kuwa Ujenzi wa miundombinu hiyo unaendelea vizuri na utakamilika kwa wakati kama ilivyoelekezwa.
Amesema kukamilika kwa Ujenzi wa Mapipa hayo mapya kutaongeza ufanisi wa kuhifadhi mafuta mengi zaidi tofauti na ilivyo sasa na kwa upande wa Flow Meter kutapunguza foleni za Meli za Mafuta Bandarini.
Baada ya ziara hiyo Mhe. Kapinga alipata fursa ya kuzungumza na Bodi ya Wakurugenzi wa Wakala huo Pamoja na Menejimenti ambapo Pamoja na mambo mengine ameulekeza wakala huo kueleza Umma majukumu wanayofanya katika kuwa hudumia watanzania.
Sambamba na hilo amewataka PBPA kutumia njia mbalimbali ikiwemo Vyombo vya Habari, Mikutano pamoja na Semima kwa watu wa makundi tofauti ili taarifa zao ziwafikie wananchi wote kwa haraka na wakati sahihi.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya PBPA, Mhandisi Lutengano Mwakahesya Pamoja na Mtendaji Mkuu wa PBPA, Erasto Simon wamemueleza Naibu Waziri huyo kuwa wamepokea maelekezo yote na kuahidi kuyafanyia kazi.
Katika ziara hiyo Naibu Waziri ameambatana na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Athumani Mbuttuka, pamoja na Viongozi wengine waandamizi kutoka Wizara ya Nishati na PBPA.
Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Judith Kapinga akizungumza na Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Wakala wa Uagizaji wa Mafuta kwa Pamoja (PBPA) wakati wa ziara yake ya kikazi katika Wakala huo, Jijini Dar es salaam.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Athuman Mbuttuka akizungumza na Wajumbe wa Bodi ya Wakala wa Uagizaji wa Mafuta kwa Pamoja (PBPA) Wakati ziara ya kikazi ya Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Judith Kapinga (Hayupo pichani) alipotembelea Wakala hiyo, Jijini Dar es salaam.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakala wa Uagizaji wa Mafuta kwa Pamoja(PBPA) Mha. Lutengano Mwakahesya akieleza maendeleo ya kazi zinazofanywa na Kampuni hiyo wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Judith Kapinga (hayupo Pichani) iliyofanyika Jijini Dar es salaam.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Uagizaji Mafuta kwa Pamoja (PBPA) Erasto Simon akieleza mafanikio na kazi zinazofanywa na Kampuni hiyo wakati wa ziara ya kikazi ya Mhe. Judith Kapinga iliyofanyika Jijini Dar es salaam.
Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Judith Kapinga(katikati) akitembelea na kukagua Miundombinu ya Upakuaji wa Mafuta ya aina yote yanayoingia na kutoka nchini wakati wa ziara yake ya kikazi katika Wakala huo, Jijini Dar es salaam
Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Judith Kapinga akizungumza na Wajumbe wa Bodi na Menejimenti ya Wakala wa Uagizaji wa Mafuta kwa Pamoja (PBPA) wakati wa ziara yake ya kikazi katika Wakala huo, Jijini Dar es salaam.
Picha inayoonesha Mapipa Mpya yanayojengwa kwa ajili ya kuhifadhi Mafuta yanayomilikiwa na Kampuni ya Uhifadhi wa Mafuta (TIPER.)
Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Judith Kapinga (wa nne toka kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na Wajumbe wa Bodi ya Wakala wa Uagizaji wa Mafuta kwa Pamoja (PBPA) wakati wa ziara ya kikazi Jijini Dar es salaam.