WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi Mashimba Ndaki,akizungumza wakati wa uzinduzi wa Bodi ya Wakurugenzi ya Bodi ya Nyama nchini uliofanyika jijini Dodoma.
WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi Mashimba Ndaki,akifafanua jambo kwa washiriki wa uzinduzi wa Bodi ya Wakurugenzi ya Bodi ya Nyama nchini uliofanyika jijini Dodoma.
KATIBU Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulia Sekta ya Mifugo Bw.Tixon Nzunda,akizungumza wakati wa uzinduzi wa Bodi ya Wakurugenzi ya Bodi ya Nyama nchini uliofanyika jijini Dodoma.
MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi ya Bodi ya Nyama Tanzania (TMB) Bw.Clemence Tesha,akitoa shukrani baada ya kuchaguliwa kuwa mwenyekiti wakati wa uzinduzi wa Bodi ya Wakurugenzi ya Bodi ya Nyama nchini uliofanyika jijini Dodoma.
Msajili wa Bodi ya Wakurugenzi ya Bodi ya Nyama Tanzania (TMB) Dkt.Daniel Mushi,akizungumza wakati wa uzinduzi wa Bodi ya Wakurugenzi ya Bodi ya Nyama nchini uliofanyika jijini Dodoma.
WAJUMBE wa Bodi ya Wakurugenzi ya Bodi ya Nyama wakimsikiliza Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mashimba Ndaki (hayupo pichani) wakati wa uzinduzi wa Bodi ya Wakurugenzi ya Bodi ya Nyama nchini uliofanyika jijini Dodoma.
…………………………………………………………..
Na Alex Sonna-DODOMA
WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi Mashimba Ndaki,amezindua Bodi ya Wakurugenzi ya Bodi ya Nyama nchini huku akiitaka kusimamia soko la nyama ndani na nje ya nchi.
Waziri Ndaki ameyasema hayo jijini Dodoma wakati akizindua Bodi ya Wakurugenzi ya Bodi ya Nyama nchini.
Waziri Ndaki amewataka kwenda kusimamia soko la nyama ndani na nje ya nchi ili kuwezesha ukuaji wa soko la nyama pamoja kuongeza mauzo.
‘Tunakupongeza Mhe Waziri kwa kutuamini tunakuahidi tutafanya kazi kwa weledi kwa kufuata Sheria,taratibu na kanuni ili tuweze kusimamia vyema mapato’amesema Bw.Tesha