Featured Kimataifa

MAREKANI KUPELEKA UKRAINE NDEGE HATARI ZISIZO NA RUBANI

Written by mzalendoeditor

Marekani inatuma ndege 100 zisizo na rubani nchini Ukraine kama sehemu ya msaada mkubwa wa kijeshi uliotangazwa na utawala wa Biden, linasema shirika la habari la Associated Press, likimnukuu afisa wa Marekani “anayefahamu uamuzi huo”.

Chanzo hicho cha jeshi la Marekani, ambacho kilizungumza kwa sharti la kutotajwa jina, kilisema mfumo wa silaha unaojadiliwa ni Switchblade 300 – silaha inayovaliwa na mkoba inayojulikana na vikosi vya Marekani kama “ndege ya kamikaze”.

Maafisa wa Bunge la Congress waliiambia NBC News mfumo wa makombora umeundwa kwa ajili ya “mashambulio ya wazi ” na unaweza kushambulia kwa usahihi kutoka mbali moja kwa moja hadi kwenye lengo lake.

Silaha hizo – ingawa ni za muundo wa Urusi – zinamilikiwa na baadhi ya wanachama wa Nato wa Ulaya na kwa hivyo zinaonekana kuwa rahisi kujumuishwa katika jeshi la Ukraine, kulingana na AFP.

Kulingana na takwimu, karibu wanajeshi 15,000 wa Soviet walikufa katika vita vya Afghanistan (1979-89), karibu wanajeshi 13,000 wa Urusi walikufa katika vita vya Chechnya, na idadi ya vifo vya Urusi huko Syria imeorodheshwa katika mamia.

About the author

mzalendoeditor