Featured Kitaifa

WIKI YA HUDUMA ZA FEDHA KITAIFA KUPUNGUZA KIWANGO CHA UMASIKINI

Written by mzalendo
Kamishna wa Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha, Dkt. Charles Mwamwaja (katikati), akizungumza na wanahabari kuhusu Maadhimisho ya Tatu ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa, yatakayotoa elimu kwa umma kuhusu umuhimu wa kutumia huduma rasmi za fedha ili kujikwamua kiuchumi na kupunguza kiwango cha umasikini nchini, yatakayofanyika tarehe 20 hadi 26 Novemba, 2023 katika viwanja vya Sheikh Amri Abeid, jijini Arusha. Kulia ni Meneja Msaidizi Idara ya Mawasiliano Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Bi. Noves Moses na Kushoto ni Mrajisi Msaidizi wa Vyama vya Ushirika Mkoa wa Arusha, Bi. Grace Masambaji.
Na Joseph Mahumi na Farida Ramadhani, WF – Arusha.
 
Wizara ya Fedha kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa Sekta ya Fedha nchini wameandaa Maadhimisho ya Tatu ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa yatakayotoa elimu kwa umma kuhusu umuhimu wa kutumia huduma rasmi za fedha ili kujikwamua kiuchumi na kupunguza kiwango cha umasikini nchini.
 
Hayo yameelezwa jijini Arusha na Kamishna wa Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha, Dkt. Charles Mwamwaja alipokutana na kuzungumza na waandishi wa habari kuhusu maadhimisho hayo yatakayofanyika tarehe 20 hadi 26 Novemba, 2023 katika viwanja vya Sheikh Amri Abeid, jijini humo.
 
Alisema kutokana na Utafiti wa FinScope wa mwaka 2023 nchini, ni asilimia 53.8 tu ya nguvu kazi wanatumia huduma rasmi za fedha ambapo kundi kubwa la Watanzania halifaidiki na huduma hizo hivyo kukosa fursa za kuboresha maisha yao kupitia shughuli mbalimbali za kiuchumi ambazo zingewawezesha kuchangia katika kukuza Pato la Taifa.
 
“Serikali inakusudia ifikapo mwaka 2025 takriban asilimia 80 ya wananchi watakuwa wamepata uelewa wa masuala ya fedha ikiwemo benki, bima na mifuko ya uwekezaji”, alibainisha Dkt. Mwamwaja.
 
Alisema maadhimisho hayo ni utekelezaji wa Mpango Mkuu wa Maendeleo ya Sekta ya Fedha wa Mwaka 2020/21 – 2029/30 ambapo elimu kwa umma ni moja ya maeneo ya kipaumbele katika utekelezaji wa Mpango huo.
 
“Madhimisho hayo pamoja na mambo mengine yanalenga kuwajengea wananchi uelewa kuhusu matumizi sahihi ya huduma za fedha, fursa zinazopatikana katika Masoko ya Fedha kupitia elimu ya fedha pamoja na namna bora ya kusimamia fedha”, alisema Dkt. Mwamwaja.
 
Aliongeza kuwa maadhimisho hayo yanalenga kuwaunganisha wananchi, wajasiriamali na wadau wengine ili waweze kutumia fursa mbalimbali zinazotolewa na sekta ya fedha katika kukuza na kuimarisha biashara zao
 
Aidha, aliwakaribisha wananchi wa Arusha na mikoa ya jirani kushiriki maadhimisho hayo ambayo yanafanyika bila kiingilio chochote.
 
Kwa upande wa wadau wengine ambao watashiriki kutoa elimu na huduma katika maadhimisho hayo wamesema kuwa maandalizi ya maadhimisho hayo yamekamilika na wapo tayari kutoa huduma.
 
Maadhimisho hayo yanatarajiwa kuzinduliwa rasmi na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa siku ya Jumatano ya tarehe 22 Novemba, 2023.
 
 
Kamishna wa Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha, Dkt. Charles Mwamwaja (katikati), akizungumza na wanahabari kuhusu Maadhimisho ya Tatu ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa, yatakayotoa elimu kwa umma kuhusu umuhimu wa kutumia huduma rasmi za fedha ili kujikwamua kiuchumi na kupunguza kiwango cha umasikini nchini, yatakayofanyika tarehe 20 hadi 26 Novemba, 2023 katika viwanja vya Sheikh Amri Abeid, jijini Arusha. Kulia ni Meneja Msaidizi Idara ya Mawasiliano Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Bi. Noves Moses na Kushoto ni Mrajisi Msaidizi wa Vyama vya Ushirika Mkoa wa Arusha, Bi. Grace Masambaji.
 
Kamishna wa Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha, Dkt. Charles Mwamwaja, akizungumza na wanahabari kuhusu Kitaifa yatakayotoa elimu kwa umma kuhusu umuhimu wa kutumia huduma rasmi za fedha ili kujikwamua kiuchumi na kupunguza kiwango cha umasikini nchini, yatakayofanyika tarehe 20 hadi 26 Novemba, 2023 katika viwanja vya Sheikh Amri Abeid, jijini Arusha.
 
 
Meneja Msaidizi Idara ya Mawasiliano Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Bi. Noves Moses, akizungumza na wanahabari kuhusu Maadhimisho ya Tatu ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa, ambapo Benki Kuu pamoja na taasisi zingine za fedha zitashiriki ili kutoa elimu ya fedha kwa wakazi wa mkoa wa Arusha katika viwanja vya vya Sheikh Amri Abeid, jijini humo, kuanzia tarehe 20 hadi 26 Novemba, 2023.
 
 
Mrajisi Msaidizi wa Vyama vya Ushirika Mkoa wa Arusha, Bi. Grace Masambaj, akizungumza na wanahabari akitoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi katika Maadhimisho  ya Tatu ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa, ambapo vyama vya ushirika vya kifedha (Saccoss) vitashiriki katika maonesho hayo kutoa elimu na ushauri kwa wakazi wa mkoa wa Arusha, na maeneo mengine nchini wakaohudhuria kwenye Maonesho hayo, katika viwanja vya vya Sheikh Amri Abeid, jijini humo, kuanzia tarehe 20 hadi 26 Novemba, 2023.
 
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Arusha)

About the author

mzalendo