Featured Kitaifa

KIWANDA CHA NGOZI KILIMANJARO KUCHOCHEA FURSA ZA AJIRA

Written by mzalendo

 

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii Mhe.Fatuma Toufiq akizungumza kwenye majumuisho ya ziara ya kamati hiyo Novemba 12, 2023 kwenye Kiwanda cha bidhaa za ngozi Kilimanjaro (KLICL), kushoto ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana ,Ajira na Wenye Ulemavu Mhe.Prof.Joyce Ndalichako.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe.Prof. Joyce Ndalichako akiwa na Naibu Waziri wa Ofisi hiyo, Mhe. Patrobas Katambi na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii Mhe.Fatuma Toufiq wakiangalia viatu vinavyozalishwa kwenye Kiwanda cha bidhaa za ngozi Kilimanjaro (KLICL)

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii, Mhe. Fatuma Toufiq akiwa Wajumbe wa Kamati wakimsikiliza mmoja wa wataalamu wa Kiwanda cha bidhaa za ngozi Kilimanjaro (KLICL).

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Joyce Ndalichako akitoa maelezo ya awali kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii kuhusu Kiwanda cha bidhaa za ngozi Kilimanjaro (KLICL).

Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Patrobas Katambi akitoa ufafanuzi wa hoja za wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii katika ziara ya kamati iliyofanyika Novemba 12, 2023 kwenye Kiwanda cha bidhaa za ngozi Kilimanjaro (KLICL).

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), CPA Hosea Kashimba akitoa ufafanuzi wa hoja za wajumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii katika ziara ya kamati hiyo ya kukagua maendeleo ya Kiwanda cha bidhaa za ngozi Kilimanjaro (KLICL).

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe.Prof. Joyce Ndalichako akiangalia mkoba wa ngozi unaozalishwa kwenye Kiwanda cha bidhaa za ngozi Kilimanjaro (KLICL).

Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Patrobas Katambi akiangalia soli ya kiatu inayozalishwa kwenye Kiwanda cha bidhaa za ngozi Kilimanjaro (KLICL).

Na Mwandishi Wetu, KILIMANJARO

KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii imeridhishwa na maendeleo ya Mradi wa Kiwanda cha Bidhaa za Ngozi Kilimanjaro (KLICL) na kueleza kwamba uwekezaji huo utachochea upatikanaji wa ajira pamoja na kuondokana na uagizaji wa viatu visivyo na ubora nje ya nchi.

Akizungumza Novemba 12, 2023 baada ya kukagua kiwanda hicho kilichopo Manispaa ya Moshi, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Fatuma Toufiq amempongeza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kusimamia kwa dhati dhana ya uchumi wa viwanda na kwamba soko la ndani la viatu likiwa kubwa, uagizaji viatu kutoka nje ya nchi visivyo na ubora wa utapungua.

Kwa upande wake, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Prof. Joyce Ndalichako, ameahidi serikali itaendelea kufanyia kazi ushauri wa kamati kwa kuwa kipaumbele kikubwa cha Rais Samia ni kuleta ustawi wa watanzania.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Ofisi hiyo, Mhe. Patrobas Katambi amesema suala la soko la viatu limeendelea kuimarika na kwa sasa kuna taasisi nyingi za serikali zinachukua viatu katika kiwanda hicho na mikakati ikiendelea kuhamasisha taasisi zingine kuchangamkia viatu hivyo ambavyo vina ubora unaotakiwa.

Awali, Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma(PSSSF), CPA Hosea Kashimba, amesema kiwanda hicho kinamilikiwa kwa asilimia 86 na mfuko huo, Jeshi la Magereza linamiliki asilimia 14 na uwekezaji wake hadi utakapokamilika unakadiriwa kufikia Sh. Bilioni 152.96.

About the author

mzalendo