Featured Kitaifa

BREAKING NEWS:DKT TULIA RAIS WA MABUNGE DUNIANI

Written by mzalendo

Spika wa Bunge la Jamahuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson amechaguliwa kuwa Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) katika uchaguzi uliofanyika leo Oktoba 27, jijini Luanda nchini Angola.

Dkt. Ackson amechaguliwa kwa kupata kura 172 kati ya kura 303 zilizopigwa na anarithi mikoba ya rais aliyemaliza muda wake, Duarte Pacheco kutoka Ureno aliyekuwa rais wa IPU kwa mihula mitatu.

Dkt. Tulia anakuwa rais wa 31 wa IPU na mwanamke wa kwanza kutoka Afrika kushika wadhifa huo.

About the author

mzalendo