Featured Kimataifa

JAMAA AJERUHIWA VIBAYA KWA KUNG’ATWA NYETI ZAKE NA JIRANI WA KIKE

Written by mzalendoeditor
Mwanaume mmoja katika kaunti ya Kakamega anapokea matibabu baada ya kushambuliwa vibaya na mwanamke.
Kulingana na ripoti, mwanaume huyo kwa jina Anthony alikuwa amekimbia katika boma la jirani yake ambapo ndugu wawili walikuwa wakipigana.
Alijaribu kuwatenganisha wakati mwanamke aliyekuwa katika vita hivyo alipoachana na kakaake na kumrukia jamaa ambaye alijikaribisha katika kualikwa kusuluhisha mzozo huo.
Inasemekana mwanamke huyo alimng’ata jamaa nyeti zake huku akimwacha na majeraha mabaya.
Mwathiriwa alisema alijaribu kuvumilia maumivu hayo lakini hakuweza, akamjulisha jirani yake ambaye alimkimbiza hospitalini.
 
“Yule dada alikuwa anapigana na kakaake, alipomwachia kaka yake alikuja na kuning’ata, moja kwa moja alinishukia na sikuweza kukabiliana naye, nilijaribu kujizuia na maumivu lakini yote yalishindikana,” alisema Anthony.
Jirani yake, kaka mkubwa wa ndugu hao wawili, alimpeleka mwathirika hospitalini.
 
“Nilikutana na Anthony na nilipomuuliza kwa nini anajikunja kwa maumivu akaniambia kuna mwanamke amemng’ata, nilichukua hatua ya kumkimbiza hospitali,” alisema jirani huyo.

About the author

mzalendoeditor