Featured Michezo

WAZIRI MKUU AWAHAMASISHA WANANCHI KUSHIRIKI KATIKA MICHEZO

Written by mzalendoeditor

Waziri Mkuu na Mbunge wa Ruangwa Kassim Majaliwa akizungumza baada ya kushiriki mbio za Ruangwa Marathon zilizofanyika mjini Ruangwa.

 Na.Mwandishi Wetu.

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amewataka wananchi kwenye maeneo mbalimbali nchini washiriki katika michezo kwa kuwa michezo ni ajira, uchumi na huimarisha afya.

“Tunapa faida nyingi kwa kufanya michezo, tushiriki katika michezo pamoja na kukimbia riadha kwa kuongeza vipaji tulivyonavyo kwani tukishindana tunapata na zawadi. Michezo ni uchumi. “ 

Mheshimiwa Majaliwa ameyasema hayo leo (Jumamosi, Septemba 9, 2023) baada ya kuzindua Ruangwa Marathon katika kiwanja cha Kilimahewa, wilayani Ruangwa Lindi.

Aidha, Waziri Mkuu amesema amemshukuru Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa maboresho makubwa aliyoyafanya katika sekta ya afya nchini ikiwemo na wilaya ya Ruangwa.

Amesema Serikali imefanya uwekezaji mkubwa katika maeneo ya kutolea huduma za afya kwa kujenga zahanati, vituo vya afyfa na hospitali ya wilaya ambayo inavifaa tiba vya kisasa.

Mbio hizo za hisani ambazo zimefanyika kwa mara ya kwanza wilayani Ruangwa zimehudhuriwa na wanariadha mbalimbali wanaoliwakilisha Taifa katika mashindano ya mbio za kimataifa.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Molel amesema mbio hizo za marathon ni nzuri kwa sababu mazoezi yanasaidia katika kupambana na magonjwa yasiyoambukiza.

Dkt. Molel amemshukuru Waziri Mkuu kwa kukubali kuwa mgeni rasmi katika mbio hizo za hisani zilizokuwa na lengo la kukusanya fedha kwa ajili ya kununulia vifaa tiba wilayani Ruangwa.

Pia, Dkt. Molel ameishukuru Serikali kwa kuboresha huduma za afya ambapo kwasasa asilimia 97 ya wagonjwa waliokuwa wanapelekwa nje ya nchi kwa matibabu wanatibiwa nchini.

Waziri Mkuu na Mbunge wa Ruangwa, Kassim Majaliwa na Mkewe Mary Majaliwa (kushoto kwake) wakishiriki katika mbio za Ruangwa Marathon kwa ajili ya kuchangia vifaa tiba zilizofanyika Ruangwa, Septemba 9, 2023. Kulia kwake ni Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Damas Ndumbaro. Kulia ni Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel na kushoto na Mkurugenzi wa Wasafi Media, Nasib Abdul maafufu  Diamond Platnum.

Waziri Mkuu na Mbunge wa Ruangwa, Kassim Majaliwa na Mkewe Mary Majaliwa (kushoto kwake) wakishiriki katika mbio za Ruangwa Marathon kwa ajili ya kuchangia vifaa tiba zilizofanyika Ruangwa, Septemba 9, 2023. Kulia kwake ni Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Damas Ndumbaro na kushoto ni Mkurugenzi wa Wasafi Media, Nasib Abdul maarufu Diamond Platnum. 

Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa akizungumza katika mbio za Ruangwa Marathon zilizofanyika mjini Ruangwa

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary wakishirki  mazoezi  ya viungo baada ya mbio za Ruangwa Marthon zilifanyika mjini Ruangwa, Septemba 9, 2023.  Wengine kutoka kushoto ni Naibu Waziri wa Afya, Dkt Godwin Mollel, Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Damas Ndumbaro na Mkurugenzi wa Wasafi Media, Nasib Abdul maarufu Diamond Platnum.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary Majaliwa wakianzisha mbio za Ruangwa Marathon zilizofanyika mjini Ruangwa.

Mkurugenzi wa Wasafi Media na Balozi wa Namungo FC, Nasib Abdul maarufu Diamond Platnum akizungumza baada ya kushiriki mbio za Ruangwa Marathon zilizofanyika mjini Ruangwa

Waziri Mkuu na Mbunge wa Ruangwa Kassim Majaliwa akizungumza baada ya kushiriki mbio za Ruangwa Marathon zilizofanyika mjini Ruangwa.

Waziri Mkuu ambaye pia ni Mbunge wa Ruangwa, Kassim Majaliwa akimvalisha medali mshindi wa kwanza wa mbio za Kilomita 21 (half Marathon) – wanawake za Ruangwa Marathon, Jackline  Sakilu  zilizofanyika mjini Ruangwa, Septemba 9, 2023. Katikati ni mshindi wa pili wa mbio hizo Faluna Matanga.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja washinda watatu wa mbio za kilomita 21 (halfu marathon) za Ruangwa Marathon – wanaume zilizofanyika mjini Ruangwa Septemba 9, 2023. Katikati ni mshindi wa kwanza Joseph  Panga, kulia ni mshindi wa pili Hamis Athumani na kushoto mshindi wa tatu Nestory Stephene.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimshukuru Ekuzi Kusula  maarufu Mzalenzo  Halisi ambaye alitembea kwa mguu kutoka Dar es salaam hadi Ruangwa mkoani Lindi kuhamasisha Tamasha la Wasafi  lililofanyika Ruangwa  mjini.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary Majaliwa wakiwapungia wananchi walioshiriki mbio za Ruangwa Marathon mjini Ruangwa.

Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

About the author

mzalendoeditor