WAPINZANI wa Simba katika Michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika timu ya RSB Berkane FC ya Morocco wameanza vyema kwa kupata ushindi kibabe wa mabao 5-3 dhidi ya US Gendarmerie National ya Niger.
RS Berkane walianza mchezo kwa kasi mnamo dakika ya 18 Fekkak Mouad alifunga bao la kwanza na katika dakika ya 20 Fekkak Mouad alirudi kambani kwa mara ya pili.
Dakika ya 25 RSB Berkane walipata bao la tatu kupitia kwa Bahri Charki mabao hayo yaliwapekeka mapumziko wakiwa kifua mbele.
Kipindi cha pili wageni waliingia kwa kujiamini na kuanza kushambulia kwa kasi na dakika ya 49 walipata kupitia kwa Adebayor Victorien na dakika ya 52 walipata bao la pili likifungwa na Boubacar Hassan.
RS Berkane walipata bao la nne bao likifungwa na Lukombe Chadrack dakika ya 65 na Larbi Najji alipigilia msumari wa tano huku wakiendelea kujiuliza wageni walipata bao la tatu dakika ya 81 likifungwa na Adebayor Victorien.
Kwa matokeo hayo RSB Berkane wanaongoza kundi D wakiwa na pointi 3 sawa na Simba waliopo nafasi ya pili wakiwa na pointi 3 wakiwa tofauti ya mabao huku nafasi ya tatu ikishikwa na US Gendarmerie na Asec Mimosas wakishika nafasi ya mwisho katika kundi hilo.