Featured Kitaifa

RAIS SAMIA ATAKA WAKUU WA MIKOA KUWAJIBIKA

Written by mzalendoeditor

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi mbalimbali wakati akifunga Mafunzo ya Wakuu wa Mikoa pamoja na Makatibu Tawala wa Mikoa katika Chuo cha Uongozi cha Mwalimu Nyerere, Kibaha kwa Mfipa mkoani Pwani tarehe 27 Agosti, 2023. 
 Wakuu wa Mikoa pamoja na Makatibu Tawala wa Mikoa wakisikiliza kwa makini hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan wakati akifunga Mafunzo yao yaliyofanyika katika Chuo cha Uongozi cha Mwalimu Nyerere, Kibaha kwa Mfipa Mkoani Pwani tarehe 27 Agosti, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisaini Kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika Chuo cha Uongozi cha Mwalimu Nyerere, Kibaha kwa Mfipa Mkoani Pwani tarehe 27 Agosti, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amewaagiza  Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa kwenda kufanya kazi kuendana na mabadiliko ya dunia.  

Rais Samia ametoa agizo hilo leo wakati akifunga mafunzo ya viongozi hao kwenye  hafla iliyofanyika katika Chuo cha Uongozi cha Mwalimu Nyerere. 

Aidha, Rais Samia amewataka viongozi hao kuwa wepesi kukabiliana na mabadiliko  hayo ili kuendana na mfumo wa kidunia wa kisiasa na kiuchumi bila kusubiri maelekezo kutoka juu. 

Vile vile, Rais Samia amewataka viongozi huo kujiamini na kuwa na hoja ya kutetea  maamuzi wanayoyafanya kwa maslahi ya wananchi na taifa kwa ujumla kwa  kuzingatia miongozo, kanuni na sheria. 

Rais Samia pia amewataka kuhakikisha usalama wa vijana kwa kusimamia miradi  inayowahusisha ambayo mingi hutumika kupenyeza ajenda zinazopotosha maadili  ya vijana na utamaduni wa taifa. 

Kwa upande mwingine, Rais Samia amewaagiza viongozi hao kuacha kupuuza  wananchi hivyo wawatumikie kwa kuwahudumia na kushughulikia kero,  malalamiko na mahitaji yao.  

Hali kadhalika, Rais Samia amewataka watumishi serikalini katika idara tofauti  kwenye ngazi za mikoa kutumia fedha za maendeleo zinazotolewa kwa maslahi ya  wananchi.  

About the author

mzalendoeditor