Featured Kitaifa

WAZIRI NDALICHAKO AWAASA VIJANA WENYE ULEMAVU KUCHANGAMKIA MAFUNZO YA KUKUZA UJUZI

Written by mzalendoeditor

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako akizungumza na wanafunzi wa mafunzo ya uanagenzi katika Chuo cha Sayansi na Teknolojia Mbeya, leo Agosti 23, 2023 jijini Mbeya.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako leo Agosti 23, 2023 akimsikiliza kijana mwenye Uziwi (wa kwanza kushoto) ambaye ni Mwanafunzi wa fani ya Kompyuta katika Chuo cha Sayansi na Tekinolojia Mbeya (MUST)

Na. Mwandishi wetu Mbeya

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako ametoa wito kwa vijana wenye ulemavu kuchangamkia fursa za mafunzo ya kukuza ujuzi zinazotolewa na Serikali kupitia Ofisi hiyo ili wajikwamue kiuchumi.

Prof. Ndalichako akizungumza Agosti 23, 2023 alipotembelea wanafunzi wa mafunzo ya hayo katika Chuo cha Sayansi na Teknolojia Mbeya, amesema Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amedhamiria kuhakikisha kunakuwepo na elimu jumuishi ili kuwapa kipaumbele watu wenye ulemavu kupata ujuzi utakaowasaidia kujikwamua kiuchumi.

Aidha, amewataka vijana kuchangamkia fursa za mikopo inayotolewa na Halmashauri pamoja na mfuko wa Maendeleo ya Vijana uliopo chini ya Ofisi hiyo ili kupata mitaji itakayowasaidia kujiajiri kupitia ujuzi walioupata kwenye mafunzo hayo.

Amewasihi vijana kulinda amani, umoja, mshikamano na kuwa mstari wa mbele katika kueleza jitihada zinazofanywa na serikali ya Awam ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan.

About the author

mzalendoeditor