Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana, akizungumza na Mkulima wa Pamba Ndg Joseph Alipopita kuangalia shmba la Kilimo Cha Pamba ,akitokea katika Mkutano wa wananchi katika Kijiji cha Laini, Halmashauri ya Wilaya ya Itilima mkoani Simiyu.(Picha na Fahadi Siraji CCM)
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Akipiga Ngoma ya mbina wakati Wa Mkutano wa wananchi katika Kijiji cha Laini, Halmashauri ya Wilaya ya Itilima mkoani Simiyu.(Picha na Fahadi Siraji CCM)
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana, akizungumza mamia ya wananchi katika Kijiji cha Laini, Halmashauri ya Wilaya ya Itilima mkoani Simiyu (Picha na Fahadi Siraji CCM)
Na Mwandishi Wetu, Itilima
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara Abdulrahman Kinana amewaeleza wananchi wa Itilima jinsi serikali itakavyotatua changamoto ya bei ndogo ya pamba nchini na uvamizi wa tembo katika makazi ya wananchi.
Kinana ametoa kauli hiyo jana Julai 28, 2023 katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kata ya Laini A wilayani Itilima Mkoa wa Simiyu akiwa ziara ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM, uhai wa Chama na kusikiliza changamoto za wananchi.
Akiwa mkoani humo Kinana alipokea malalamiko ya wananchi hasusan wakulima wa pamba kwamba wanatumia gharama kubwa kulima zao hilo, lakini changamoto inayowakabili ni bei ndogo, hivyo walimuomba awasaidie kufikisha kilio chao kwa Chama na serikali upatikane ufumbuzi wa bei ya pamba.
Kinana baada ya kuwasikiliza wakulima hao aliowapa nafasi ya kuuliza maswali, alisisitiza kwamba kuondoa changamoto ya bei ndogo ya pamba, serikali kuu ijitahidi kutengeneza viwanda vya kutengeneza nyuzi, kuchakata pambana na kutengeneza nguo kusiwe na ulazima wa kupeleka pamba nje ya nchi.
Miongoni mwa changamoto hizo, ni pamoja na Bei ndogo ya pamba, upatikanaji wa pembejeo bora za kilimo na uvamizi wa tembo katika makazi na maeneo ya shughuli za binadamu.
Akijibu changamoto hizo alisisitiza kuwa amechukua changamoto hizo na atakwenda kuzungumza na viongozi wanaohusika.
Hata hivyo Kinana alisema baadhi ya hatua ambazo zitasaidia kukabiliqna na changamoto katika zao la pamba ni muhimu kujenga viwanda vya nyuzi na nguo.
Pia, Kinana alisema ni muhimu kila mkulima ahakikishe analima kisasa, akitoa mfano mkoani Singida alisema kuna mkulima wa pamba anayelima kisasa katika heka moja anapata kilo 1,000.
“Mkuu wa Mkoa wenu (Yahaya Nawanga), mwaka huu amelima pamba katika kila heka moja amepata kilo 500, wewe unayelima hapa (Itilima) kwa utaratibu wako, heka moja unapata kilo 150, hamuwezi kufanana kwa mapato.
“Sasa ni kazi ya serikali kuwaleta watalaamu wawafundishe wananchi walime kilimo cha kisasa. Kuhusu malipo ya pamba nitakwenda kukutana na Waziri wa Kilimo Hussein Bashe.Tutazungumza kwa nini watu wasilipwe fedha kila wanapouza.
“Sio wanauza halafu wanalipwa nusu, halafu wanalipwa tena robo na baadaye robo nyingine, fedha inakuwa haina thamani,”valisema Kinana alipokuwa akizungumza na wananchi waliojitokeza kwa wingi katika mkutano huo uliofanyika katika Kijiji cha Laini A.
Kuhusu malalamiko ya wananchi kuvamiwa na tembo ambao wamekuwa wakisababisha wananchi kupoteza maisha, Kinana alisema amekaa na viongozi wa ngazi mbalimbali wa wilaya, mkoa na maofisa wa uhifadhi wanyamapori kuzungumzia tatizo la wananchi kuvamiwa na kuuliwa na tembo.
“Tumezungumza kuhusu fidia kwa watu wanaokufa, tumezungumzia mipaka kati ya wananchi na hifadhi, nitakaporudi nitazungumza na Waziri wa TAMISEMI, Waziri wa Maliasili na Utalii pamoja na Waziri wa Ardhi hili jambo hili lifanyiwe kazi.” alisema.