Featured Kitaifa

MAKAMU WA RAIS AFUNGUA WIKI YA MAADHIMISHO YA JKT

Written by mzalendoeditor

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akikata utepe kuashiria Uzinduzi wa Mnara wa Miaka 60 ya JKT uliopo katika eneo la Makao Makuu ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Chamwino mkoani Dodoma. Uzinduzi huo ni katika Ufunguzi wa Wiki ya Maadhimisho ya Miaka 60 ya JKT. Tarehe 01 Julai 2023. (Wengine katika Picha ni Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Innocent Bashungwa, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Faraji Mnyepe, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa Meja Jenerali Rajabu Mabele pamoja na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama Mhe. Vita Kawawa)

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akipanda mti aina ya Mstafeli katika eneo la Makao Makuu ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Chamwino mkoani Dodoma wakati wa Ufunguzi wa Wiki ya Maadhimisho ya Miaka 60 ya JKT. Tarehe 01 Julai 2023.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akizindua Mnara wa Miaka 60 ya JKT uliopo katika eneo la Makao Makuu ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Chamwino mkoani Dodoma. Uzinduzi huo ni katika Ufunguzi wa Wiki ya Maadhimisho ya Miaka 60 ya JKT. Tarehe 01 Julai 2023. (Wengine katika Picha ni Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Innocent Bashungwa, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Faraji Mnyepe, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa Meja Jenerali Rajabu Mabele pamoja na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama Mhe. Vita Kawawa).

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akitembelea mabanda mbalimbali ya maonesho ya bidhaa zinazozalishwa na Jeshi la Kujenga Taifa na Wadau wengine kutoka nje ya JKT yaliopo katika viwanja vya Suma JKT House eneo la Medeli Mashariki Jijini Dodoma wakati wa Ufunguzi wa Wiki ya Maadhimisho ya Miaka 60 ya JKT. Tarehe 01 Julai 2023.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akiwapa Samaki chakula katika moja ya Bwawa la kufugia Samaki lilibuniwa na Jeshi la Kujenga Taifa wakati akitembelea maonesho ya Miaka 60 ya JKT yanayofanyika katika viwanja vya Suma JKT House eneo la Medeli Mashariki Jijini Dodoma wakati wa Ufunguzi wa Wiki ya Maadhimisho ya Miaka 60 ya JKT. Tarehe 01 Julai 2023.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akihutubia wakati wa Ufunguzi wa Wiki ya Maadhimisho ya Miaka 60 ya JKT mara baada ya kutembelea mabanda ya maonesho ya bidhaa mbalimbali zinazozalishwa na JKT na Wadau wengine kutoka nje ya JKT katika viwanja vya Suma JKT House eneo la Medeli Mashariki Jijini Dodoma leo tarehe 01 Julai 2023.

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa JKT Mhe. Innocent Bashungwa,akizungumza wakati wa Ufunguzi wa Wiki ya Maadhimisho ya Miaka 60 ya JKT mara baada ya kutembelea mabanda ya maonesho ya bidhaa mbalimbali zinazozalishwa na JKT na Wadau wengine kutoka nje ya JKT katika viwanja vya Suma JKT House eneo la Medeli Mashariki Jijini Dodoma leo tarehe 01 Julai 2023.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akipokea zawadi tuzo kutoka kwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Innocent Bashungwa mara baada ya Ufunguzi wa Wiki ya Maadhimisho ya Miaka 60 ya JKT iliofanyika mkoani Dodoma leo tarehe 01 Julai 2023.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akiwa katika picha ya pamoja na wawakilishi wa Vijana wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) wakati wa Ufunguzi wa Wiki ya Maadhimisho ya Miaka 60 ya JKT mkoani Dodoma leo tarehe 01 Julai 2023. (Wengine katika Picha ni Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Innocent Bashungwa, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Faraji Mnyepe, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa Meja Jenerali Rajabu Mabele pamoja na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama Mhe. Vita Kawawa)

Na. Gideon Gregory, Dodoma.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango amefungua rasmi maonyesho ya kilele cha maadhimisho ya miaka 60 ya Jeshi la Kujenga Taifa JKT Maadhimisho yanayoenda sambamba na kuonyesha shughuli mbalimbali zinazofanywa na JKT huku akibainisha kuridhishwa na maandalizi ya maonyesho hayo.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa maonyesho hayo yanayofanyika katika viwanja vya Jengo la Shirika la uzalishaji mali la Jeshi la Kujenga Taifa SUMA JKT Medel East Dkt. Mpango amesema JKT imejipanga kikamilifu na anaamini maonyesho hayo yatakuwa chachu ya mabadiliko kwa wananchi katika kazi na bidhaa zinazozalishwa na JKT.

“Nimepita katika mabanda mengi nimeona kazi mnazozifanya kwa kweli nimeridhishwa kwa jinsi maonyesho haya mlivyoyaandaa na kazi na bidhaa mnazozizalisha kwa kweli mmejipanga wito wangu mjitangaze zaidi kwa wananchi kazi zenu ni nzuri sana” amesema.

Amemtaka Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Bi. Rosemarry Senyamule kuwaalika Wakuu wa Mikoa Jirani kuja kujifunza katika maonyesho hayo na kuhamasisha wananchi wao kuhudhuria maonyesho hayo yenye tija kubwa kwa mageuzi ya sekta mbalimbali hapa nchini.

Amesema JKT imekuwa na mchango mzuri katika kuinua pato la taifa na kwa ushirikiano na wadau wengine katika shughuli za kimaendeleo hapa nchini na kuwataka kuungana na wadau mbalimbali katika kuinua zaidi ubora wa bidhaa na teknolojia wanazotumia.

Katika hatua nyingine amesema Serikali inatambua juhudi kubwa za JKT katika malezi kwa vijana kwa kuimalisha maadili, uzalendo na umoja wa kitaifa kwa vijana na mchango wao katika sekta ya kilimo na kuwa na uhakika wa chakula hapa nchini.

Ameongeza kuwa “Katika juhudi zenu za uzalishaji mali na ulinzi kwa taifa ni vema mkatilia mkazo na katika utunzaji wa mazingira na kuhamasisha wananchi katika utunzaji wa mazingira kwa kudhibiti utupwaji wa taka za plastiki ovyo.

Kwa upande wake Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa JKT Mhe. Innocent Bashungwa amesema Serikali itaendelea kuiwezesha JKT katika kutekeleza majukumu yake ya malezi kwa vijana kwa kupanua uwezo wa kuchukua vijana hasa wa kwa mujibu wa sharia na  kupitia Shirika lake za uzalishaji mali SUMA JKT katika kutekeleza miradi yake mbalimbali kwa ufanisi.

Waziri Bashungwa pia ameahidi kutekeleza kwa ufanisi mkubwa maelekezo yote yaliyotolewa na Makamu wa Rais na maagizo ya Mkuu wa Nchi hasa katika kujitosheleza kwa chakula na ziada kuinufaisha taifa.

Awali Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa JKT Meja Jenerali Rajabu Mabele amesema maonyesho hayo yamelenga katika kutangaza kazi kubwa ambayo inafanywa na JKT ikiwa ni kutimiza miaka 60 tangu kuanzishwa kwake Julai 10, 1963 ikiwa na lengo la kutoa malezi bora kwa vijana.

Amesema tangu kuanzishwa kwake kwa kiasi kikubwa wamefikia malengo ya kuanzishwa kwake katika malezi kwa vijana na uzalishaji mali hasa kwa kuchangia katika pato la taifa kupitia kazi wanazozifanya katika kuzalisha bidhaa na kazi mbalimbali kupitia miradi mikubwa wanayotekeleza.

Amesema katika maonyesho hayo bidhaa mbalimbali zinazozalishwa na JKT zitaoneshwa na kazi mbalimbali mbali na bidhaa na kazi hizo pia kutakuwa na maonyesho ya wanyama pori ikiwa ni juhudi za kuunga mkono jitihada za serikali katika kuvitangaza vivutio mbalimbali vya kitalii.

Amesema kupitia wiki ya kilele cha maadhimisho ya miaka 60 ya kuanzishwa kwake shughuli hizo zitaambatana na mabonanza ya michezo mbalimbali, kutembelea watu wenye uhitaji na kuchangia damu kwa ajili ya kuokoa maisha ya wenye uhitaji.

Katika hatua nyingine Makamu wa Rais Dkt Philip Mpango amezindua  Mnara ambao ni kielelezo kuwa  JKT  imetimiza miaka 60 tangu kuanzishwa kwake Julai 10, 1963 lengo ni jamii itambue juhudi kubwa zinazofanywa na JKT.

About the author

mzalendoeditor